• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

Elimu

HUDUMA ZA ELIMU

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo pia imejikita katika kutoa huduma bora za elimu ya Msingi na Sekondari.

ELIMU MSINGI

Halmashauri ina jumla ya shule za Msingi 39.  Kati ya shule hizo 32 ni za Serikali na 7 ni za binafsi.  Shule hizi zina jumla ya wanafunzi 21,833 wakiwemo wavulana 11,088 na wasichana 10,745.  Pia shule zina jumla ya walimu 668 wakiwemo wanaume 164 na wanawake 504.


UTEKELEZAJI WA ELIMU BURE

Jamii wakiwemo wazazi wameipokea sera ya Serikali ya Elimu bure kwa furaha kwani elimu bila malipo ni kielelezo cha usawa katika utoaji wa fursa sawa ya elimu.  Kutokana na utekelezaji wa sera hii nzuri, idadi ya wanafunzi wa elimu ya awali na Darasa la kwanza walioandikishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ni 7300 kama jedwali linavyoonesha hapa chini;


Aidha, kwa kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi 2017 Serikali imetuma jumla ya Shillingi 166,558,000 kugharamia elimu bure kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:-


UFAULU WA WAHITIMU WA DARASA LA VII


Kiwango cha ufaulu katika Halmashauri kimekuwa kimeongezaka kwa kasi kutoka asilimia 70.9 hadi kufikia asilimi 78.1 kwa mwaka 2016 kama inavyonekana katika jedwali lifuatalo


MIUNDOMBINU

(a) Madarasa na Vyoo

Kiwango kikubwa cha uandikishaji kilichosababishwa na mpango wa Serikali wa Elimu bila malipo umesababisha upungufu mkubwa wa madarasa, vyoo na miundombinu mingine katika shule zetu.

Jedwali kuonyesha hali ya vyumba vya madarasa na vyoo:


(b)Madawati:

Halmashauri inahitaji madawati yapatayo 7695 yaliyopo ni 8675 ambapo kuna ziada ya madawati 980 sawa na asilimia 104% ya utekelezaji kama inavyoonyesha:-


Wadau mbalimbali waliofanikisha zoezi la madawati ni pamoja na wafuatao:-

NA.JINA LA MDAUIDADI YA MADAWATI

1.Mkuu wa Mkoa wa Pwani122

2.Mkuu wa Wilaya Bagamoyo50

3.Subashy Patel600

4.Dr. Reginald Mengi250

5.Vijiji/Jamii ya Bagamoyo2638

6. TASAF 69

7.Waheshimiwa Wabunge537

8.P4R55

9.TANAPA150

10.Mzinga10

10.Simba Motors100

JUMLA4581


Aidha Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara walichanga posho zao Tshs.13, 140,000/= ambazo zilitumika kugharamia uchanaji na usafirishaji wa mbao pcs 3,164 ambazo zilitumika kutengeneza madawati 1200 yaliyotoka Kiwanda cha Mdau Subashy Patel.


CHANGAMOTO

•Upungufu wa vyumba vya madarasa 291 uliotokana na uandikishaji mkubwa, hivyo kusababisha msongamano wa wanafunzi darasani.

•Upungufu wa nyumba za walimu


UFUMBUZI

•Pamoja na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa Halmashauri kwa kushirikiana na jamii tunaendelea kujenga vyumba vya madarasa katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri. Miradi hii inatekelezwa katika kata za;

i)DUNDA

ii)NIANJEMA

iii)KISUTU

iv)MAGOMENI

v)MAKURUNGE

vi)KIROMO

vii)ZINGA

viii)KEREGE

ix)MAPINGA

x)YOMBO

xi)FUKAYOSI


ELIMU SEKONDARI


Halmashauri ya Bagamoyo ina jumla ya Shule za Sekondari 21 zikiwemo Shule za Serikali 09 na za watu binafsi/Taasisi 12. Halmashauri Ina jumla ya wanafunzi 10,716 kati yao Shule za Serikali ni 5,006 (Wavulana 2,483 na Wasichana 2,523) na Shule za binafsi/Taasisi ni Wanafunzi 5,710 (Wavulana 2,591 na Wasichana 3,119).

Idadi ya Walimu katika Shule za Serikali ni 463 ambapo waalimu wa masomo ya Sayansi ni 78 na wa masomo ya Sanaa 385.  Aidha Halmashauri ina upungufu wa walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati 61.

Waliochaguliwa kidato cha kwanza katika Halmashauri ya Bagamoyo mwaka 2017 ilikuwa 1,536 (Wav 698 na Was 838) na walioripoti hadi March 2017 ni 1,446 (Wav 658 Was 788) sawa na asilimia 96 na wasioripoti ni 90 (wav 40 was 50) sawa na asilimia 6. Halmashauri inaendelea kufuatilia wanafunzi ambao hawajaripoti.


UFAULU WA MITIHANI YA TAIFA

Maendeleo ya ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa kwa kidato cha nne na sita ni ya wastani na imeendelea kuimarika. Katika kidato cha nne ufaulu kwa mwaka 2012 ilikuwa ni 43% wakati mwaka 2016 ni 77.5%. Hili ni ongezeko la 34.5% ya kutoka mwaka 2012. Ufaulu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 ulikuwa ni asilimia 90% wakati mwaka 2016 ni asilimia 96% sawa na ongezeko la 6%. Halmashauri yetu pia imeendelea kutoa shule bora katika ngazi ya taifa ambapo kwa mwaka 2016 shule ya sekondari Ahmes imeshika nafasi ya kwanza (1) Kitaifa katika shule zenye wanafunzi chini ya 40 na Marian wasichana ilishika nafasi ya nne (4) kitaifa katika shule zenye wanafunzi zaidi ya 40 kwa mtihani wa kidato cha nne na mwaka 2016 kushika nafasi ya sita (6) kitaifa katika mtihani wa kidato cha sita.


HALI YA MADAWATI

Katika mwaka 2016 Halmashauri ya Bagamoyo ilijikita katika utengenezaji wa madawati. Kabla ya agizo la Mhe. Rais, Halmashauri ilikuwa na meza 3,547 na viti 3,536 ambapo mahitaji yalikuwa ni meza 4,789 na viti 4,789. Hivyo na kufanya upungufu wa meza 1,242 na viti 1,253. Baada ya utekelezaji wa agizo la mhe Rais Halmashauri hadi kufikia Desemba 2016 ilikuwa na jumla ya meza 5,002 na viti 5,016 hii inafanya madawati yote yaliyokarabatiwa na mapya kuwa jumla ya meza 1,455 na viti 1,480.

Mwanzo wa mwaka 2017 kulikuwa na mabadiliko ya takwimu za madawati kutokana na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza tofauti na wale waliomaliza kidato cha nne 2016. Ongezeko hilo limesababisha mahitaji ya madawati kwa shule za Halmashauri kuwa 5,507 yaliyopo 5,016 na upungufu kuongezeka hadi 491


UJENZI WA MADARASA NA MATUNDU YA VYOO

Shule ya Sekondari Kerege iliyopo Halmashauri ya Bagamoyo kata ya Kerege ina mradi wa Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa, hali ya utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua ya   Msingi, pia kuna ukarabati wa miundombimu ya vyoo kwa shule ya Dunda chanzo cha pesa kikiwa ni fedha za ‘Performance For Results’(P4R) na Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule ya Sekondari ya Bagamoyo, chanzo cha pesa kikiwa ni michango ya Wadau mbali mbali, Ofisi ya mkuu wa Wilaya na Serikali kupitia fedha za ( P4R).‘Performance For Results’.


UJENZI WA VYUMBA VYA MAABARA

Halmashauri ya Bagamoyo inahitaji kuwa na vyumba vya maabara 27 kwa masomo ya sayansi katika shule 9 za Sekondari. Maabara 19 zilizokuwa zinapungua tayari zilishajengwa na kuezekwa. Kazi inayoendelea sasa ni utafutaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara.


ELIMU YA JUU

Halmashauri pia ina vyuo vinavyotoa taaluma mbalimbali katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada. Vyuo hivi ni pamoja na chuo kikuu cha Marian (MARUCO), chuo cha uongozi wa Elimu (ADEM), chuo cha ukutubi (SLADS), chuo cha sanaa na utamaduni (TASUBA), chuo cha uvuvi Mbegani (FETA), chuo cha uuguzi, Taasisi ya Hisabati na Sayansi Afrika (AIMS) na chuo cha kilimo Kaole. Vyuo hivi vimetoa nafasi kubwa ya masomo kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita wa shule zetu za sekondari.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC NDEMANGA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI IFM...

    June 28, 2025
  • WEHESHIMIWA MADIWANI WAFANYIWA TAFRIJA YA KUWAAGA....

    June 20, 2025
  • MILIONI 8.13 YATOLEWA KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU...

    June 20, 2025
  • MKURUGENZI BAGAMOYO ZIARA YA KIKAZI...

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo