• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
    • Baraza la Madiwani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Baraza la Madiwani
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • UKARIBISHO
        • service one
        • what we do
        • Utalii
        • Kaole Snake Park
        • Kaole Mamba Ranch
        • Completed
        • Elimu
        • Afya
        • Maji
        • Caravan Serai
        • Education
        • Ukaguzi wa Ndani
        • TAARIFA YA O& OD
        • Miradi iliyopendekezwa
        • Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Ujenzi
        • Mfuko wa Jamii
        • Mifugo na Uvuvi
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Idara ya Maji
        • Sheria ndogo za Halmashauri
        • Ardhi na Mipango Miji
        • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
        • Sheria
        • Ufugaji Nyuki
        • Usafishaji na Mazingira
        • Fedha na Biashara
        • Election Unit
        • Ugavi na Manunuzi
        • Maeneo ya Uwekezaji
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kupata Fomu Mbalimbali
        • Madiwani
        • Baraza la Madiwani
        • Orodha ya Wahe.Madiwani
        • Kamati za kudumu za Halmashauri
          • Elimu, Afya na Maji
          • Fedha, Uogozi na Mipango
          • Kamati ya UKIMWI
          • Kamati ya Maadili
          • Uchumi, Ujenzi, Mipango miji na Mazingira
        • Ratiba za Vikao vya Kisheria
        • Ratiba
          • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
          • Ratiba ya Vikao vya Wahe. Madiwani
        • Mpango Mkakati
        • Bajeti ya Halmashauri
        • Mkataba wa huduma kwa Mteja
        • ZABUNI MBALI MBALI ZA UWAKALA
    • Baraza la Madiwani
  • Idara na Vitengo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Works
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Usafi na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Elimu Msingi
    • Kitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Election Unit
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2018/2019
    • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MPYA
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

Idara ya Maji


IDARA YA MAJI


Idara ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaongozwa na Mkuu wa Idara Ndg; Jabiri Mussa Kayilla

Simu Na. 0754 678 237.


Idara ya Maji ina watumishi 9 kati ya hao watumishi wenye taaluma ya Maji ni 7.

Jukumu kubwa la Idara ya Maji ni kuwezesha wananchi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupata huduma ya maji safi, salama na ya kutosha katika umbali usiozidi mita 400 kwa mahitaji yao binafsi na mahitaji mengine ya kiuchumi Kama ilivyoelezwa kwenye sera ya maji ya mwaka 2002.

Aidha Idara hii inafanya kazi kwa kuzingatia sheria ya maji Na.11 ya mwaka 2009 inayohusu usimamizi wa rasilimali za maji na sheria Na.12 ya mwaka 2009 inayohusu usimamizi wa utoaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira, Idara hii pia hufanya kazi kwa kuzingatia malengo yaliyoko kwenye MKUKUTA Na II, Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020, Dira ya taifa ya mwaka 2025.


Majukumu ya Ofisi ya Mhandisi wa Maji (W)


(a )     Kuhakikisha kuwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wanapata huduma ya maji safi na  salama katika umbali usiozidi mita 400 kwa kuongeza idadi ya vituo vya kuchotea maji(DPs)

(b.)Kusimamia ukarabati na ujenzi wa miradi kama inavyoelekezwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji na mipango ya Halmashauri.

(c.)Kuratibu zoezi la manunuzi ya miradi ya maji katika vijiji vyote kwa kushirikiana na Kitengo cha Manunuzi

(d.)Kuratibu usimamizi na ufuatiliaji wa miradi kwa kushirikiana na wataalam wa kamati maji na usafi wa mazingira wilaya (CWST)

(e.)Kuandaa taarifa za kila mwezi, robo ya mwaka na mwaka na kuziwasilisha kwa wakati katika maeneo/vikao husika

(f.)Kuandaa bajeti ya idara kwa kila mwaka kwa kufuata mpango wa bajeti na vipaumbele vya jamii na halmashauri.

(g.)Kusimamia uanzishwaji na usajili wa Vyombo huru vya watumiaji maji (COWSOs) kwa kushirikiana na Msajili


 MIRADI

Idara ya maji toka mwaka 2010 imekuwa ikitekeleza programu ya maendeleo ya sekta ya maji ambayo imesisitizwa na kutekelezwa chini ya mradi wa matokeo makubwa sasa (BRN)  ambapo miradi tisa ilipangwa kutekelezwa katika vijiji vya YOMBO, TALAWANDA, KITAME, MAPINGA, KIHARAKA, MILO,KIDOGOZERO/KITONGA, MATAYA NA SAADANI. Miradi hiyo ilitekelezwa chini ya program ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya kwanza. Utekelezaji wa miradi hii ulisimamiwa na  Halmashauri ya Bagamoyo kabla ya mgawanyo wa Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo.

Miradi iliyotekelezwa halmashauri ya bagamoyo ni, YOMBO, KITAME, MAPINGA, KIHARAKA NA MATAYA.


MIRADI TUNAYOSHIRIKIANA NA WADAU WENGINE


Idara ya maji inashirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa huduma ya maji safi na salama katika halmashauri ya Bagamoyo.


I.Mamlaka ya Maji safi na maji taka chalinze (CHALIWASA) katika vijiji vya  mkenge, Mwavi, Fukayosi, Kidomole na  Makurunge.

II.Mamlaka ya maji safi na taka Dar - es-salaam (DAWASA) kwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika mji wa Bagamoyo mpaka sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa tanki la maji la lita 6,000,000 na uboreshaji wa mtandao wa bomba katika mitaa ya Matimbwa,Yombo, Kiromo, Mataya, Zinga, Kerege na Mapinga.

III.Ofisi ya makamu wa Raisi katika mradi wa Mabadiliko ya tabia ya nchi katika ujenzi wa visima 10 vya kisasa katika kata za Nianjema, Kiromo, Dunda na Zinga pamoja na kujenga mfumo wa kuhifadhia maji ya mvua katika shule ya sekondari ya Kingani.

IV.Time to help kutoka Ugiriki katika ujenzi wa visima 6

V.Kanisa la Perispiani missionaries kutoka Marekani katika ujenzi wa visima 6 katika vijiji vya Matimbwa, Kondo, Buma, Zinga na SUnguvuni

VI.Islamic foundation katika ujenzi wa visima 16


Aidha tutaendelea kushirikiana na wadau wengine watakaojitokeza katika ili kuweza kuwahudumia wananchi


MIONGOZO


Katika kutekeleza majukumu ya Idara ya Maji inatumia sheria,sera na miongozo mbalimbali.


Baadhi ya nyaraka hizo ni:-


I.Project Implementation Manual (PIM )

II.District Operation Manual (DOM)

III.Project Operation Manual (POM)

IV.Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002

V.Sheria Na. 11 ya Rasilimali za Maji ya mwaka 2009

VI.Sheria Na. 12 ya Maji Safi vijijini na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009



BODI ZA WATUMIA MAJI.

Idara ya maji imeendelea kukabiliana na changamoto ya miradi mingi ya maji  iliyoko vijijini kutofanya kazi vizuri  kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo kutosimamiwa vizuri na kukosa matengenezo muhimu. Kutokana na  dhana kuwa jukumu la  kuwapatia  wananchi huduma ya maji ni la Serikali pekee, Upungufu huo umesababisha kuhitajika  kwa mpango thabiti na endelevu wa uratibu na usimamizi wa utoaji wa huduma hii katika ngazi ya halmashauri ya kuunda Bodi za watumia maji na  kuzipa mafunzo pamoja na  kusajili Bodi hizo.


MSAJILI WA BODI ZA WATUMIA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA


kupitia Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.12 ya mwaka 2009. Halmashauri za Wilaya, ina mamlaka ya kuteua msajili na kusimamia mchakato mzima wa usajili chini ya Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira, iliyoanza kutumika rasmi tarehe 1.8.2009.

Katika Halmashauri ya Bagamoyo Msajili wa bodi hizi ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Bagamoyo.


UUNDAJI NA USAJILI WA VYOMBO VYA WATUMIAJI MAJI


(i) Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Kijiji au Kamati ya Maji kwa kushirikiana na Wataalam Washauri  au Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Wilaya itaitisha kikao cha awali ili kuweka bayana na kujadili wazo la kuunda chombo cha watumiaji maji kwa miradi iliyokwishakamilika, inayoendelea kujengwa au itakayojengwa.


(ii) Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Kijiji itaafikiana kuhusu kuunda chombo cha watumiaji maji na uamuzi huo utawasilishwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji.


(iii) Washauri au Timu ya Wataalam wa Maji na Usafi wa Mazingira ya Wilaya wataelimisha wananchi katika vikao mbalimbali vitakavyoandaliwa, kuhusu umuhimu wa kuunda vyombo vya watumiaji maji vilivyosajiliwa kisheria, aina mbalimbali za vyombo vya watumiaji maji, kuwaongoza na kutoa ushauri katika mchakato wa kuchagua aina ya chombo wanachokipenda, taratibu na hatua za usajili kwa kila aina ya chombo. Chombo cha watumiaji maji kitaanzishwa baada ya wananchi kukubaliana kwa pamoja kwa kuzingatia masharti au vigezo vinavyotawala katika aina ya chombo kitakachochaguliwa.


(iv) Mkutano wa wanakijiji wote utaitishwa ili kuamua kwa pamoja, kwa mujibu wa walio wengi, kuunda aina ya chombo cha watumiaji maji wanachoona kinawafaa kwa mujibu wa maelekezo ya wataalam wa wilaya. Mkutano huo utateua kamati ya muda itakayokuwa na viongozi waanzilishi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia watakaosimamia uundaji wa chombo cha watumiaji maji.


Endapo chombo cha watumiaji maji kitahusisha zaidi ya kijiji kimoja, maamuzi ya wananchi katika kila kijiji yatajadiliwa katika kamati ya muungano yenye wawakilishi wa wananchi kutoka kila kijiji.


(v) Viongozi waanzilishi watasimamia shughuli ya kuandaa rasimu ya katiba na kanuni za chombo kilichopendekezwa.(rejea katiba ya mfano ambayo imeambatanishwa kwenye mwongozo huu).  Kwa mujibu wa mwongozo huu, uandaaji wa rasimu ya katiba na kanuni utamshirikisha Mhandisi wa Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mwanasheria wa Halmashauri husika.


(vi) Viongozi waanzilishi walioteuliwa watawasilisha rasimu ya katiba na kanuni kwenye mkutano mkuu wa wanakijiji wote ili kujadiliwa na kupitishwa na mkutano huo.


Iwapo chombo kinachotarajiwa kuundwa kitahusisha kijiji zaidi ya kimoja, rasimu na katiba ya chombo itawasilishwa katika mkutano wa pamoja utakaowajumuisha wawakilishi wa wananchi kutoka vijiji husika, ambao kwa pamoja watafikia maamuzi.


(vii) Pia, viongozi waanzilishi watawasilisha nakala ya rasimu ya katiba na kanuni kwenye kikao cha maendeleo ya kata kwa taarifa, kumbukumbu na pia ili kuthibitisha kutokuwepo kwa pingamizi ndani ya kata. Hii itawezesha kubaini kuwepo au kutokuwepo kwa jumuiya kama ile inayopendekezwa ndani ya kata.


(viii) Baada ya kupitishwa kwa rasimu za katiba na kanuni,  mwenyekiti na katibu wa kamati ya muda watawasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri rasimu ya katiba, kanuni na nyaraka zote zinazotakiwa kwa ajili ya uundaji wa chombo cha watumiaji maji, ili kipate ridhaa ya Halmashauri. Mkurugenzi wa Halmashauri ana uhuru wa kufanya ukaguzi au uchunguzi wowote anaouhitaji kupitia wataalam wake ili kujua hali halisi, kabla ya kuwasilisha ombi la kuunda chombo kwenye kamati au vikao husika kwa ajili ya kupata ridhaa.


(x) Mkurugenzi wa Halmashauri atakiandikia barua chombo husika kilichoundwa, akionyesha kuwa Halmashauri imetoa ridhaa ya kuundwa kwa chombo husika katika kijiji/vijiji kilichowasilisha maombi hayo, akiambatanisha majina ya viongozi waanzilishi (Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina) wa chombo husika  kwa kuzingatia matakwa ya katiba na atatoa nakala kwa Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kijiji.


(xi) Kufikia hatua hii, chombo cha watumiaji maji tayari kitakuwa kimeundwa kulingana na katiba na kanuni walizojiwekea, tayari kwa hatua za usajili.


USAJILI WA VYOMBO VYA WATUMIAJI MAJI


(i) Viongozi wa chombo cha watumiaji maji watawasilisha fomu ya maombi ya kusajili chombo cha watumiaji maji kwa Msajili na kutoa nakala kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Afisa Mtendaji wa Kata, wakiambatanisha katiba na kanuni ya chombo hicho na muhtasari wa mkutano mkuu wa wanakijiji/wanavijiji wote pamoja na majina ya wajumbe waliohudhuria na sahihi zao na nakala ya barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri inayoonyesha kuwa Halmashauri imeridhia uundaji wa chombo hicho.


(ii) Waombaji watalipia ada ya usajili wa chombo cha watumiaji maji kama itakavyopangwa na Msajili wa Vyombo vya Watumiaji Maji wa Halmashauri.


(iii) Msajili atahakiki uhalali wa chombo cha watumiaji maji kilichofuzu vigezo vilivyotakiwa kwenye usajili na kutoa mapendekezo au ushauri kwa chombo ambacho hakikufuzu ili kizingatie vigezo na  kiweze kufuzu.


(iv) Wananchi watafahamishwa kuhusu matokeo ya uhakiki iwapo maombi yao yanafuzu vigezo vilivyowekwa au kama yanahitaji maboresho kabla ya kusajiliwa.


(v) Msajili atatoa hati ya kisheria ya usajili kwa chombo cha watumiaji maji kilichofuzu vigezo vilivyotakiwa ili kitambulike kisheria na kuweza kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa mujibu wa sheria.


(viii) Msajili atatoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu maombi yaliyopokelewa, kuhakikiwa, kukubaliwa na kusajiliwa ama kukataliwa.


(ix) Waombaji ambao maombi yao yamekataliwa wanayo haki ya kukata rufaa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri baada ya kulipa ada kama itakavyopangwa na msajili.



Matangazo

  • RATIBA YA MHE. MKUU WA MKOA KUTEKELEZA TAARIFA YA MHE. WAZIRI WA ARDHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI MAPINGA SIKU.. February 20, 2023
  • NAFASI ZA KAZI. 1. WAANDIKISHAJI WAPIGA KURA 167. 2. WAANDIKISHAJI WA AKIBA 167. September 11, 2019
  • Tangazo la nafasi za kazi Halamashauri ya wilaya Bagamoyo 2020. January 24, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA BVR OPERATOR BAGAMOYO DC TAREHE 09/01/2020 February 07, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI WA HALMASHAURI BAGAMOYO AFUNGA MAFUNZO YA UWAWA..

    March 22, 2023
  • MAFUNZO YA UWAWA YAENDELEA BAGAMOYO..

    March 21, 2023
  • MAFUNZO YA UWAWA KUSAIDIA KUTEKKELEZA MALENGO YA ELIMU BAGAMOYO..

    March 20, 2023
  • DC-BAGAMOYO WATAOCHEZEA HAKI YA WANAWAKE NA WATOTO SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU..

    March 08, 2023
  • Angalia zote

Video

KAULI YA RAIS MAGUFULI WAKATI AKIZINDUA BARABARA YA BAGAMOYO - MSATA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 023 - 2440164

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo