• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BAGAMOYO WAANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS

Posted on: December 7th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeanza kutimiza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Wananchi wa Bagamoyo, hasa vikundi vya wajasiriamali wanawake na vijana wananufaika na mradi mkubwa wa ufugaji wa kuku wazazi toka kampuni ya AKM glitters iliyopo Kitongoji cha Yombo.

Katika kulisimamia na kutimiza agizo hilo, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii, kwa kushirikiana na kampuni ya AKM glitters, imefanya mafunzo maalum ya siku mbili, kwa viongozi wa vikundi 8 vya wanawake, vinavyojishughulisha na ufugaji wa Kuku, na kuwapa elimu juu ya ufugaji bora wa kuku wazazi na namna watakavyonufaika na mradi huo ambao kwa sasa unatekelezwa na kampuni ya AKM glitters.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri, Mkuu wa Idara ya amendeleo ya jamii, Ndg. Julius Mwanganda amesema, wanatarajia baada ya mafunzo hayo, vikundi shiriki kuanza ufugaji wa kuku wazazi watakaopewa na kampuni ya AKM glitters, na kila kikundi kitawezeshwa kuku 500 kwa kuanzia, huku nusu ya gharama za kununua kuku hao ikilipwa na Halmashauri kwa vikundi vitakavyokuwa na sifa, kupitia uwezeshwaji wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya mikopo inayotolewa kwa Wanawake na Vijana.

“Tumezungumza na kampuni ya AKM glitters inayojishughulisha na ufugaji wa kuku wazazi huko Yombo, na wamekubali kushirikiana na Halmashauri, kuwezesha vikundi vya wanawake wanaojishughulisha na ufugaji wa Kuku, Kampuni ya AKM itatoa punguzo kwa wanavikundi la asilimia 10, huduma za ugani, chakula cha kuku kwa mwezi mmoja na vyombo vya kulishia kuku, huku Halmashauri ikiwawezesha wanavikundi hao nusu ya gharama ya ununuzi wa vifaranga vya kuku wazazi toka kampuni ya AKM glitters” Amesema Ndg. Mwanganda.

Baada ya kukamilika kwa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku wazazi, yaliyoendeshwa kwa siku mbili kwa wanavikundi wanawake, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kampuni ya AKM wamefanya ziara ya kuvitembelea vikundi vyote 8 ili kujiridhisha kama vikundi hivyo vinakidhi vigezo vya kupatiwa msaada huo.

Agizo la kusimamia na kuhakikisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo hususani Vikundi vya Wanawake vinanufaika na mradi wa kuku wazazi unaoendeshwa na kampuni ya AKM glitters iliyopo Yombo, lilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa katika ziara ya kutembelea shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, ambapo katika ziara hiyo pia alitembelea mradi wa kuku wazazi unaoendeshwa na kampuni ya AKM glitters uliopo Kata ya Yombo. Ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa Mwezi wa kumi, mwaka huu 2018.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo