• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BAGAMOYO YAZINDUA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Posted on: May 1st, 2018


Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo  imefanya zoezi la uzinduzi wa chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa Wasichana wenye umri wa miaka 14 Wilayani humo.

Uzinduzi huo umefanyika katika kliniki ya mama na mtoto iliyopo katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo mapema asubuhi ya Aprili 30, 2018.

Chanjo hiyo ambayo ni endelevu inawalenga watoto wa kike wote wenye umri wa miaka 14 pamoja na wale waliofikisha umri huo katika kipindi cha mwezi Machi na Aprili mwaka huu.

Akizindua zoezi hilo, Katibu tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Erica Yegela, amewataka wazazi wenye wasichana wenye umri wa miaka 14 kuhakikisha wanawapeleka watoto wao Hospitalini hapo, pia katika Vituo vya Afya na Zahanati vilivyopo katika Wilaya hiyo ili wapatiwe chanjo hiyo muhimu itakayowalinda dhidi ya maradhi ya Saratani ya mlango wa kizazi.

Bi. Yegela pia akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa watoto wa kike kutojihusisha na vitendo vya ngono mara baada ya kupatiwa chanjo hiyo kwani vitendo hivyo ndio chanzo kikubwa cha Saratani ya Mlango wa kizazi huku wanaume wakiathirika kwa kiwango kidogo.

“Serikali inatumia fedha nyingi kutibu wagonjwa wa Saratani ya shingo ya kizazi hivyo imeona ni jambo jema ianze kutoa chanjo yake ambayo ni gharama ndogo kuliko matibabu yake ili kuokoa kizazi kijacho dhidi ya maradhi hayo yanayoondoa maisha ya wanawake wengi nchini hivi sasa" Amesema Bi. Yegela.

Nae mratibu wa zoezi hilo, Dr. Mohamed Farah kwa niaba ya Mganga Mkuu Wilaya ya Bagamoyo, ameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau kwa kuwezesha zoezi la utoaji wa chanjo hii muhimu kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 Wilayani Bagamoyo ili kutokomeza maradhi ya Saratani ya mlango wa kizazi hivyo kupunguza vifo lakini pia kuwa na kizazi salama cha watoto wa kike wasio na maradhi hayo kwa miaka ijayo.

Wasichana 10 toka Shule ya msingi mwambao walipatiwa chanjo hiyo katika uzinduzi huo na chanjo hiyo sasa inapatikana hospitalini hapo hivyo wazazi na walezi wanahimizwa kupeleka mabinti zao wenye umri wa miaka 14 kupatiwa chanjo hiyo.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo