• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BAISKELI 35 KUSAIDIA USAFIRI KWA WANAFUNZI WASICHANA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI BAGAMOYO

Posted on: November 21st, 2018

Taasisi isiyo Kiserikali ya Hope for young Girls Tanzania inayotekeleza mradi wa kusaidia Wanafunzi wasichana waishio katika mazingira hatarishi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, imetoa msaada wa Baiskeli 35, kwa wanafunzi wasichana wanaosoma Shule za Sekondari Kingani, Fukayosi na Kiromo.

Msaada huo umetolewa na taasisi hiyo kwa Wanafunzi hao ambao wanaishi mbali na mazingira ya Shule wanazosoma, zilizopo katika Kata za Kiromo, Kisutu na Fukayosi, hali inayopelekea kuwa katika hatari mbalimbali hasa alfajiri wanapokua wakielekea Shuleni na walengwa wakuu ni Wasichana wenye umri wa miaka 11-19.

Mratibu wa mradi huo Bi. Salama Kikudo amesema wanatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na taasisi ya Mundo Cooperante iliyopo Madrid Hispania ambao ndio wafadhili wakuu wa mradi huo hapa Nchini.

“Tuna utaratibu wa kutembelea Shule za Msingi na Sekondari na kutoa elimu ya kujenga kujiamini na kujilinda kwa Wasichana wanaosoma katika Shule hizo, na huwa tunawapima uelewa wa masomo tuliyowafundisha kwa kuwauliza maswali ambayo wanayajibu kwa uandishi wa insha, Njia zingine za mawasiliano tunazotumia ni michezo mbali mbali” Anasema Bi. Salama Kikudo

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Afisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Julius Mwanganda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji, ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo ambao utawasaidia sana wanafunzi hao kuwahi kufika shuleni asubuhi na kurudi nyumbani wakati wa jioni, lakini pia kuwaepusha na hatari na vishawishi hususani toka kwa waendesha bodaboda ambao huwarubuni wasichana kwa kuwapa lift ili kushiriki nao kimapenzi hali inayopelekea wanafunzi wengi kukatisha masomo yao kwa kupata ujauzito.

Nae Caroline Kabile, mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kingani, akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliopokea msaada huo amesema, msaada huo umefufua matumaini  na kuwapa chachu ya kukazana katika masomo yao, kujikita zaidi katika kutia bidii ya kufanikiwa kielimu kwa kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kupelekea wao kukatiza masomo yao hivyo kushindwa kufikia ndoto zao.

Kwa takribani miaka miwili sasa Taasisi ya Hope for young girls Tanzania, inatekeleza mradi wa kusaidia wanafunzi wasichana waishio katika mazingira magumu katika mkoa wa Pwani, ikizihudumia Wilaya za Bagamoyo na Kisarawe.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo