• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BIDHAA ZA MAGENDO ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL. 25 ZATEKETEZWA

Posted on: October 2nd, 2019

Bidhaa zenye thamani ya Shilingi milioni 25, zimeteketezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitengo cha forodha Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Idara ya Afya, Usafi wa mazingira na Udhibiti wa taka ngumu pamoja na Jeshi la Polisi.

Uteketezaji huo umefanyika leo katika dampo la Sanzale lililopo Kata ya Magomeni baada ya kubainika kuwa ni za magendo, zimekatazwa kuingizwa Nchini na hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na betri dazeni 12, Matairi ya magari na pikipiki 400, Nguo za mitumba balo 9, vilainishi ‘lubricants’ lita 960, mafuta ya taa lita 300, Friji 2, kompresa za friji 12 na sabuni za unga Kilo 30. Bidhaa zote zikiwa na thamani ya jumla ya Shilingi Mil. 25,949,001/-

Ofisa Forodha wa TRA Bandari ya Bagamoyo Bw. Noel Makere akizungumza wakati wa uteketezaji huo amesema bidhaa hizo ni za magendo na zilikamatwa katika doria zinayofanywa na Ofisi yake.

“Matairi haya 400 tunayoteketeza leo yamekatazwa kabisa kuingizwa na kutumika Nchini, huku bidhaa kama friji na mitumba ni bidhaa zilizozuiwa kuingizwa Nchini. Bidhaa za betri, mafuta ya taa na vilainishi ni bidhaa tunazoteketeza kutokana na kukosa ubora wakati zinakamatwa. Amesema Makere.

Bw. Makere anaongeza kusema, “Nawasihi Wafanyabishara kuwa wazalendo na kufuata sheria na taratibu za uingizaji bidhaa Nchini hususani ulipaji wa kodi ili kuepuka usumbufu na hasara zisizo za lazima. Tumekuwa tukitoa elimu na huduma bure kwa wafanya biashara ili kuwasaidia kufanya biashara zao kwa kufuata sheria na taratibu za Nchi, pia tunashirikiana vizuri na vyombo vya Ulinzi na usalama na tumejipanga kuhakikisha hakuna bidhaa za magendo zinazopitishwa Bagamoyo ili kodi ya Serikali isipotee”.


Naye Ofisa Afya wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Mohamed Farah, aliyesimamia uteketezaji wa bidhaa hizo, amewasihi wafanya biashara kutii sheria bila shuruti na kuhakikisha bidhaa wanazoingiza Nchini hazina madhara kwa watumiaji ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi ya bidhaa zilizokosa ubora na zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo