• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BIDHAA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 93 ZAHARIBIWA

Posted on: October 2nd, 2018

Mamlaka ya mapato TRA Bagamoyo kwa kushirikiana Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Idara ya Afya na Idara ya Usafi na udhibiti wa taka ngumu, wamefanya zoezi maalumu la uteketezaji wa bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu leo tarehe 02 Oktoba, 2018.

Zoezi hilo limefanyika katika dampo la Sanzale lililopo katika Kata ya Magomeni na bidhaa zilizoharibiwa ni pamoja na mafuta ya kupikia lita 26,840, sukari kilo 46,300, mchele kilo 5,400 maziwa kilo 950 na biskuti kilo 60, zikiwa na thamani ya Tsh 93,277,368.17.

Afisa forodha wa TRA Bagamoyo, ndg. Noel Makele amesema bidhaa zilizoteketezwa ni mali ya TRA kwani walizikamatwa kama bidhaa za magendo.

“Tumefikia hatua ya kuziteketeza bidhaa hizi kutokana na kukosa ubora wakati zinakamatwa pamoja na kuhifadhiwa kwa muda mrefu zikisubiri ufuatiliaji na hatma ya kesi mbalimbali, hii imepelekea baadhi ya bidhaa kuisha muda matumizi hivyo kutofaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu” Anasema Ndg. Makele.

Nae Afisa Afya Bi. Agnes Nkingwa aliyesimamia zoezi hilo la Uteketezaji wa bidhaa amesema, zoezi hilo limefanyika chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi sura Na. 219 ya Mwaka 2003 na kanuni zake za utupaji wa vyakula visivyofaa ya mwaka 2006.

Zoezi hilo la uteketezaji wa bidhaa lilishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainabu Kawawa na lilifanikishwa chini ya usimamizi wa Wataalamu ambao ni Mkaguzi wa chakula kutoka TFDA kanda ya Mashariki, Maafisa kutoka Mamlaka ya Bandari, Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mamlaka ya Mapato Bagamoyo na Jeshi la Polisi huku njia iliyotumika kuharbu bidhaa hizo ikiwa  ni kuchanganya udongo na kuzifukia.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo