• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC-BAGAMOYO WATAOCHEZEA HAKI YA WANAWAKE NA WATOTO SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU..

Posted on: March 8th, 2023

MKOA wa Pwani, kupitia madawati ya ustawi wa Jamii na maeneo ya utoaji huduma za kijinsia katika Halmashauri yamepokea migogoro ya ndoa 689 ,matunzo 908 na migogoro inayohusu watoto wa nje ya ndoa 973 katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2022 .

Kufuatia migogoro na mashauri hayo, ndani ya jamii, Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Pwani,mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Halima Okash, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake kimkoa yaliyofanyika Bagamoyo,alitoa rai kwa wanawake kupigania haki zao ,na kusisitiza Serikali ipo nyuma yao kuchukua hatua kwa wale ambao wanajaribu kuchezea haki za mwanamke na mtoto.

Aidha, aliiasa Jamii Mkoani humo kuendelea kulinda amani ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Okash alieleza,wanawake wamekuwa injini ya mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa na wamekuwa mchango mkubwa katika kulea na kuelekeza maadili mema ya kitanzania kwa maana hiyo umoja na uzalendo uwe nguzo kimkoa na Taifa kijumla.

"Mkoa una Jumla ya kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zipatazo 546, jumla ya mashauri 2,570 yamepokelewa na kusikilizwa katika madawati ya ustawi wa jamii na maeneo mengine ya utoaji wa huduma katika Halmashauri kwa kipindi hicho, kati ya hayo migogoro ya ndoa 689,matunzo 908, watoto nje ya ndoa 973,yaliyopelekwa mahakamani 162 na yaliyohukumiwa 49"alifafanua Okash.

Kuhusu kumwezesha mwanamke,Okash alieleza, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa ulitenga kiasi cha sh Bilioni 3.6 hadi Januari 2023 ambapo Jumla ya Bilioni 1.5 zilichangiwa na kupelekwa kwenye akaunti ya wanawake, vijana na wenye ulemavu, katika fedha hizo million 750,554,502 zilitolewa kwenye vikundi hivyo.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake Mkoani Pwani Zainabu Vullu aliyataka madawati ya kijinsia kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa jamii ili kudhibiti vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Aliwataka wanawake, wawa wabunifu na kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwani ni chachu katika kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kutumia teknolojia vizuri ili kupata elimu ya kuandaa bidhaa Bora na kupata masoko.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkoani Pwani, Mariam Ulega alieleza, wameanzisha Kampuni ya Gomama ili kumwezesha kiuchumi mwanamke na amewaomba wajiunge kununua hisa .

Mariam,aliwasisitiza wanawake hao kuendelea kujiinua kimaisha na kiuchumi ili kujiongezea kipato.Mjasiriamali Rosemary Kwilasa aliishukuru Serikali kwa kutoa mikopo ya asilimia 10 katika mapato ya halmashauri ambapo kikundi Chao kilichopo Ukuni, Bagamoyo kimenufaika kwa kupatiwa milioni 8.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo