• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC KAWAWA APIGA MARUFUKU UINGIZAJI MIFUGO KIHOLELA

Posted on: September 13th, 2018

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa Vijiji na Watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu kuwa waache mara moja tabia hiyo kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina ya Wafugaji na Wakulima.

Mhe. Zainab ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo wakati wa mabaraza ya madiwani yaliyofanyika mapema wiki hii Wilayani humo.

 Mhe. Zainab alieleza kuwa wapo viongozi wanaopokea pesa toka kwa wafugaji, kisha kuwapokea kiholela katika Vijiji vyao, suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi.

 Anaongeza kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano na mikwaruzano baina yao.

“Nasema imetosha, wilaya kwasasa ina mifugo 300,000. Halmashauri ya Chalinze ina ng’ombe 240,000 na Halmashauri ya Bagamoyo ng’ombe 60, 000, Wilaya haina uwezo wa kupokea zidio la mifugo kwa sasa na kwa watendaji wa Vijiji waliokuwa wakijihusisha na uingizaji mifugo kwa kutumia njia ambazo ni kinyume cha sharia niwaonye kupitia ninyi wawakilishi wao, Wahe. Madiwani muwafikishie ujumbe huko katika Kata zenu mnazoziongoza, kuanzia sasa ni marufuku Mtendaji kuingiza mifugo kiholela katika Kijiji chake na atakaebainika kwenda kinyume na agizo hili nitamshughulikia kikamilifu” Amesema Mhe. Zainab.

Mhe. Zainab pia amesema amefanya mazungumzo na NARCO Bagamoyo waliopo katika Kata ya Vigwaza na wamesema wamekubali kutenga eneo lenye ukubwa wa heka 100,010 ambalo wamekubali kuwakodisha wafugaji wa Bagamoyo ili waweze kulisha mifugo yao kwa utaratibu wa kulipa Kiasi cha Shilingi 10,000 kwa ng’ombe mmoja kwa muda wa miezi mitatu, mitatu, utaratibu anaoamini kuwa utapunguza ongezeko la mifugo hiyo na ufugaji holela katika Wilaya ya Bagamoyo.

“Nawaomba Wahe.madiwani na watendaji tupeane ushirikiano kwa kuwafikishia ujumbe huu wa kheri kwa Wafugaji wakubwa waliopo katika maeneo yetu ili kuwashirikisha mpango huo wa NARCO ili tumalize kbisa migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya yetu ya Bagamoyo na naahidi binafsi kukutana na makundi ya wafugaji na kuzungumza nao kuhusu kuheshimu mipaka isiyowahusu na juu ya kupeleka mifugo yao NARCO“ Amesema Mhe. Zainab.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu amesema wamepokea maelekezo hayo na anaamini kuwa wataalamu, Wahe. Madiwani, Watendaji na Wananchi wote kwa ujumla watatoa ushirikiano mkubwa ili kumaliza migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Bagamoyo na kuhakikisha wanailetea Bagamoyo maendeleo na si Migogoro.

Diwani wa Kata ya Yombo, Mohamed Usinga alisema changamoto ya kuingizwa makundi ya mifugo kiholela ni kero kubwa hasa katika Kata yake lakini mpango mpya wa Mhe. Mkuu wa Wilaya anaamini utatua kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo na kuwaomba Wakulima na Wafugaji Wilayani Bagamoyo kuheshimiana, kupendana na kuishi kwa amani.  Usinga aliahidi kwa niaba ya madiwani wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kumpa ushirikiano mkuu huyo mpya wa Wilaya ili kudhibiti kero hiyo.





Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo