• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC KAWAWA AWAWEZESHA WAFANYA BIASHARA WADOGO WENYE UHITAJI MAALUM MTAJI

Posted on: June 9th, 2020

Vijana wawili wenye uhitaji maalum ambao pia ni wafanya biashara wa mafuta ya kupikia Mjini hapa, wamepokea msaada maalum wa mtaji wa Shilingi 210,000/- kila mmoja sawa na madumu 5 ya mafuta yenye ujazo wa lita 20 ili wakaendelee na biashara hiyo waliyokuwa wakifanya hapo awali kabla ya kukabiliana na changamoto ya kuishiwa mtaji.

Msaada huo umetolewa kwa vijana hao na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa Ofisini kwake hapo leo ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyowapa vijana hao kuwa atawasaidia mtaji ili waendelee na biashara zao baada ya kusimama kwa muda kwa kuishiwa mtaji.

“Leo nimewaita hapa Ofisini kwangu hawa ndg. Maneno Fadhili Maneno na ndg. Juma Mharami ambao ni wafanya biashara wadogo wa mafuta ya kupikia maarufu kama shuba shuba katika bandari yetu hii ya Bagamoyo, ili kutimiza ahadi yangu niliyowaahidi juma lililopita kuwa nitawasaidia mtaji ili waendelee na biashara zao baada ya kuishiwa mtaji kutokana na changamoto zilizokuwa zimejitokeza katika bandari yetu ya Bagamoyo zilizofanya shughuli katika bandari hiyo kusimama, changamoto ambazo zimeshafanyiwa kazi hivyo bandari kurudi katika utendaji wake wa awali hivyo ndugu zetu hawa pia wanahitajika warudi bandarini hapo kuendelea na biashara yao na leo nimewawezesha mtaji huu wa Shilingi 210,000/- kila mmoja, nendeni mkazitumie fedha hizi kwa malengo mliyojiwekea, hakikisheni zinawasaidia kibiashara na mnasimama tena kiuchumi kama ilivyokuwa awali naamini hamtaniangusha” Amesema Mhe. Zainab

Baada ya kupokea msaada huo, Mmoja wa Wafanya biashara hao Ndg. Maneno Fadhili Manenoakizungumza kwa niaba ya Mwenzake, amemshukuru sana Mhe. Zainab kwa kujitoa na kuwathamini wao na kuwatazama kwa jicho la tofauti na kuamua kuwasaidia ili nao waweze kujikwamua kiuchumi na kupata uwezo wa kuhudumia familia zao

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanya biashara Wilayani hapa Ndg. Shaban Khamsin almaarufu “Chavurugu” ambaye ameshuhudia makabidhiano hayo amesifu weledi na utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa kwa kuhakikisha wafanya biashara hao wenye uhitaji maalum kupata msaada huo utakaowawezesha kuendelea na biashara yao ya mafuta na kuendesha familia zao

“Haijapata kutokea kiongozi mwenye moyo wa upendo na kujitoa kwa wanyonge kama wewe Mheshimiwa Zainab, umetuonesha upendo na kutujali sana wana bagamoyo na msaada uliowapatia Ndg. Maneno na mwenzake Muharami ni msaada mkubwa na umetuonesha utu hasa hawa wenzetu waliokuwa wamekwama na maisha yao kusimama ama hakika tendo hili tutalikumbuka daima” Amesema Ndg. Shabani.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ametoa msaada huo ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyowapatia vijana hao wiki iliyopita, baada ya kuishiwa kabisa mtaji kutokana bandari ya Bagamoyo kusimama kufanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wafanya biashara hao wadogo wa mafuta ni wenye uhitaji maalum hivyo msaada huo utawawezesha kujikwamua toka katika changamoto za kimaisha kwa kuanza tena kufanya biashara yao ya mafuta ya kupikia wanayoagiza kutoka Unguja na kuja kuuza kwa reja reja hapa Bagamoyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo