• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC NDEMANGA AHIMIZA SWALA LA UPANDAJI WA MITI...

Posted on: November 16th, 2024

DC NDEMANGA AHIMIZA SWALA LA UPANDAJI WA MITI

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Shaibu Ndemanga amehimiza wananchi leo tarehe 16 November 2024 wakati akishiriki zaoezi la upandaji wa miti shule ya Msingi Kigongoni kuwa na utaratibu wa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kuwa swala zima la upandaji wa miti ni jukumu la kimamoja nani jambo ambalo linaleta manufaa hapo baadae kwani kupanda miti kunafaida nyingi katika mazingira huku pia akizitaka taasisi zote ziwe mfano katika swala zima la upandaji wa miti.


Vilevile  Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kampeni ya upandaji wa miti ni kampeni endelevu kwani hata Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hushiriki mazoezi ya upandaji wa miti na kuhimiza wananchi kupanda miti katika maeneno yao.


Sambamba na yote Mhe Ndemanga ametoa wito kwa wananchi kutumia mvua za vuli ambazo zimeanza  kunyesha na kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi huku akiwaomba viongozi wa ngazi za vijiji,Vitongoji na Watendaji kata kusimamia zoezi hilo  la upandaji wa miti kwa wananchi.  


Mwakilishi wa Benk ya Starndard Charter ambae ni kiongozi wa Idara ya Teknologia ndg Christopher  amesema kuwa wanazaidi ya miaka 13 katika kampeni ya kujali mazingira kwa kupanda miti kwa mkoa wa Pwani na Dar es Salaam   kwa upande wa Wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni mwaka wao wa tatu wakiwa wamefanya hivyo katika shule 5


Ameendelea kwa kusema kuwa sababu kubwa ya kuendelea na kampeni hiyo ni kwa kujua umuhimu wa mazingira kwa sasa na vizazi vinavyokuja baadae huku akisema kuwa ni wajibu wao kama benki kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahali salama huku akitoa wito kwa kuendela kutunza miti hiyo kwa  faida ya baadae.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shauri Selenda ametoa shukrani kwa wadau wa Benk ya Starndard Charter kwa kuwapatia miti 2000 na kwakushirikiana na Taasisi ya Tatedo nao wamewapatia miti 2000  na kufikia miti 4000 ambayo imepandwa katika eneo hilo la shule ya Msingi Kigongoni 


Mkurugenzi ametoa Rai kwa walimu,wananfunzi na wananchi kwa ujumla kuwa miti hiyo 4000 inatunzwa na kuhakikisha inakuwa na kuleta manufaa  ili ije isaidie baadae kutoa matunda na vivuli  kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

 


 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo