• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DED BAGAMOYO APONGEZA MRADI WA ZAO LA MCHICHA CHAMBEZI

Posted on: September 26th, 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu, amepongeza utekelezaji wa mradi wa utafiti wa mbegu bora za Mchicha unaofahamika kama “Amazing Amaranth” uliotekelezwa na Kituo kidogo cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Chambezi katika Kitongoji cha Chambezi Wilayani hapa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Fatuma Latu, aliyekuwa Mgeni rasmi katika Siku maalum ya Mkulima wa Zao la Mchicha iliyofanyika katika Kituo kidogo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI Chambezi Septemba 26, 2020.

“Niwapongeze wakulima na watafiti walioshiriki katika utekelezaji wa mradi huu wa ‘Amazing Amaranths” (Mchicha zao la kushangaza) tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2018. Mradi huu umetekelezwa katika Mkoa wa pwani na Mikoa ya kaskazini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro na kushirikisha wakulima, maafisa ugani, wauzaji wa pembejeo za kilimo na watafiti wa Kilimo. Mradi umefanikiwa kutoa matokeo ya Mbegu bora 05 za Mchicha ambazo zinafaa kulimwa katika maeneo yetu na kutuletea tija Kiafya kwa kuboresha lishe, iwapo Mchicha huo utatumika kama Chakula na Kiuchumi iwapo Mkulima atalima Mchicha kibiashara kwa kuuza kama mboga mboga ama kusindika malighafi zitokanazo na zao la Mchicha na kupata bidhaa mbalimbali kama unga wa Mchicha au vitafunwa vya Mchicha”. Amesema Mkurugenzi Fatuma.

Anaongeza Mkurugenzi Fatuma, Mchicha ni zao lisilopewa kipaumbele, lakini nawapongeza TARI Chambezi kwa kubuni mradi huu ulioleta matokeo tofauti kabisa na kuondoa dhana ya Wananchi kudhani Mchicha si zao muhimu, badala yake sasa wataanza kuona umuhimu wa zao la Mchicha linaloweza kuboresha lishe ya jamii na linapolimwa kibiashara linaweza kumtoa Mkulima katika umaskini kabisa.

“Tatizo la utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka 05, bado ni janga Nchini na takwimu za udumavu kwa sasa ni kati ya Asilimia 34 hadi 14 huku tatizo la uzito mdogo na ukondefu ni Asilimia 5, viwango hivi havikubaliki na kama Wataalam wa Kilimo na Lishe tuna wajibu wa kuhamasisha jamii kutumia vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili kuondokana na maradhi haya ya Utapiamlo, ukondefu na udumavu, bahati nzuri vyakula vyenye viini lishe hivyo vinapatikana katika zao la Mchicha ambalo kila mwanajamii ana uwezo wa kulima nyumbani na kupata chakula hiki chenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili pale tu Mchicha utakapoandaliwa kwa ubora unaotakiwa, hivyo natoa rai kwa wanajamii ya Bagamoyo na kwingineko Nchini kulipa kipaumbele zao la Mchicha ili kuondokana na utapiamlo na kuongeza kipato cha familia”. Amesisitiza Mkurugenzi Fatuma.

Nae Meneja wa kituo cha utafiti wa Kilimo Nchini TARI Mikocheni Ndg. Zuberi Bira akizungumza katika hafla hiyo amesema Lengo kuu la mradi wa “Amazing Amaranths” ni kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora wa zao la Mchicha, kuinua uchumi na kuondoa utapiamlo Nchini.

Pia Mradi unahusika na tafiti za kuboresha upishi wa Mchicha, Utoaji mafunzo kwa wadau na upatikanaji wa mbegu mpya bora za mchicha na kwamba hadi sasa mbegu 05 bora za Mchicha, zimepasishwa katika mradi huo, Mbegu hizo ni Madiira 1, Madiira 2, Nguruma, Akeri na Poli ambazo zimepandwa katika kituo hicho cha utafiti na kuonesha matokeo mazuri huku akiwaasa Wanajamii kutumia mbegu hizo na kutoa elimu kwa wengine ili watumie fursa hii ya uzalishaji wa Mchicha na kuboresha lishe katika jamii yetu.

Hafla ya maadhimisho ya siku ya Mkulima wa Zao la Mchicha, imefanyika katika kituo kidogo cha utafiti cha TARI Chambezi huku Mgeni rasmi katika siku hiyo akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu ambaye mbali ya kuzungumza na wataalam wa kilimo, Afya, lishe na Wakulima na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo pia alikagua mabanda ya maonesho ya shughuli za wajasiriamali wa bidhaa za zitokanazo na Mchicha ambapo wajasiriamali walionesha bidhaa za uji wa Mchicha, supu ya Mchicha, bisi za Mchicha, Keki ya Mchicha, Unga lishe wa Mchicha, Cerellac ya Mchicha na Mbegu bora 05 za Mchicha.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo