• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

HOSPITALI ZOTE ZA WILAYA NCHINI ZIJENGE JENGO LA KUHUDUMIA WAGONJWA WA DHARURA: UMMY MWALIMU

Posted on: September 25th, 2017


Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, ametoa  agizo kuwa Hospitali zote za Wilaya nchini ziwe na jengo maalumu la kuhudumia wagonjwa wenye dharura.

Mhe. Waziri ametoa agizo hilo leo Tarehe 25 Septemba, 2017 mjini Bagamoyo, alipokuwa katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi  ujenzi wa wodi ya wazazi na jengo la kuhudumia wagonjwa wa dharura ‘emergency care unit’ katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo.

“Naagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini, wajenge majengo ya kupokelea na kuhudumia wagonjwa wenye dharura yaani ili kuongeza wigo wa kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi wanaohitaji huduma ya haraka na dharura, nitumie fursa hii kuagiza kuwa ifikapo Tarehe 30 June, 2018 majengo hayo yawe yamejengwa kwenye kila hospitali ya Wilaya nchini”. Amesema Mh. Waziri.

Mhe. Waziri wa Afya, Bi. Ummy Mwalimu alikuwa mgeni rasmi katika uwekaji mawe ya msingi Majengo mawili yenye ghorofa moja yanayojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyin inayofanya kazi nchini, ambapo yatakapokamilika wafadhili hao pia wataweka vifaa vikiwemo vitanda na vifaa tiba kabla ya kuyakabidhi kwa matumizi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majid Mwanga amewashukuru wafadhili hao taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyin kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kwani katika Halmashauri ya Bagamoyo.

“Tunaishukuru sana Taasisi hii kwakuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali kuiletea jamii maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kuipunguzia Serikali mzigo. Taasisi hii imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo miradi ya maji kwa kuchimba visima virefu 23 na vifupi 15 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 614 na sasa wamefadhili mradi huo wa ujenzi wa wodi ya wazazi na jengo la kuhudumia wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo”. Aliongeza Mhe. Mwanga

Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akatumia fursa hiyo kuiomba Serikali kupitia Mhe. Waziri Ummy Mwalimu, kutoa msamaha wa kodi kwa vifaa tiba vitakavyoletwa na wafadhili hao kutoka nje ya nchi ili vitumike kwenye majengo hayo pindi yatakapokamilika, ili wafadhili hao waweze kuitumia fedha hiyo kununua vifaa tiba vingi zaidi.

Mhe. Kawambwa pia akaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kiasi cha Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Kerege kwani Halmashauri hiyo haikuwa na kituo cha Afya na pia akamshuru Mhe. Waziri kuridhia kituo hicho cha Afya kujengwa katika kata ya Kerege kulingana na mahitaji badala ya kujengwa katika Kata ya Dunda kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.


Mganga Mkuu Wilaya ya Bagamoyo Bi. Sylivia Mamkwe akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa Mhe.Waziri amesema huduma ya Mama na mtoto Kiwilaya imeimarika na vifo vya akina Mama wakati wa kujifungua pia vimepungua kutoka akina mama 11 Mwaka 2015 hadi akina Mama 8 Mwaka 2016.

Hivyo ujenzi wa wodi hiyo mpya ya wakina Mama itasaidia uboreshaji wa utoaji huduma ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo