• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

JAFFO AZINDUA MAJENGO MAPYA HOSPITALI YA WILAYA YA BAGAMOYO

Posted on: July 7th, 2018



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Seleman Said Jaffo amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha kuwa, hakuna kituo cha Afya katika mkoa huo kinachopata nyota sifuri katika utoaji huduma kwa Wananchi.

Mhe. Waziri Jaffo alitoa agizo hilo jana wakati alipomwakilisha Mhe. Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wodi ya wazazi na jengo huduma ya dharura katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Dhi Nureyin Islamic Foundation ya mkoani Iringa.
Jaffo akatumia fursa hiyo kusisitiza juu ya utoaji huduma bora za Afya katika vituo vyote vya Afya katika Mkoa wa Pwani na kuongeza kuwa, hakuna sababu ya kituo chochote cha Afya Nchini kushindwa kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani Serikali ya awamu ya tano, chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imefanya kazi kubwa na ya kupigiwa mfano kwa kujenga vituo vingi vya Afya kote Nchini ili kuboresha huduma ya Afya hususani huduma bora za Afya ya Mama na Mtoto, hivyo ni aibu kubwa kwa kituo cha Afya kupata nyota sifuri katika utoaji huduma kwa Wananchi, ilihali Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri katika vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na kuongeza Wataalam wa Sekta ya Afya katika Halmashauri zote Nchini.

"Mganga Mkuu Mkoa wa Pwani kama itatokea kituo chochote cha afya katika mkoa wako kikapata nyota sifuri katika utoaji huduma kwa Wananchi itabidi uje ofisini kwangu kujieleza, tusicheze na Afya za Wananchi wetu wakati Serikali inaweka mazingira mazuri katika idara hiyo, hivyo jipangeni na waganga wakuu wa Wilaya kuhakikisha hilo halitokei, " amesema Jaffo.

Mhe. Jaffo pia ameipongeza taasisi hiyo ya Dhi Nureyin kwa kuweza kuwajengea majengo hayo ya kisasa na muhimu katika mkoa huo wa Pwani.

Mbali ya kuwapongeza Dhi Nureyin kwa ujenzi huo lakini pia Mhe. Waziri Jaffo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga, kwa kuweza kutafuta ufadhili huo, na hatimaye kupata majengo hayo.
Aidha, akawataka Wahudumu wa Afya  Mkoani humo, kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa Wananchi na kuacha tabia ya kutowatolea maneno makali na lugha chafu pindi wanapohitaji huduma ya afya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kupatikana kwa majengo hayo ni ukombozi kwa Mkoa huo kutokana na ongezeko la Wananchi Mkoani humo wanaoongezeka kila kukicha.
Ndikilo aliwataka Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Afya Nchini nan je ya Nchi, kuiga mfano wa taasisi hiyo ya Dhi Nureyin kwa kushirikiana na Serikali katika kujenga na kuboresha vituo vya Afya.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyin, Sheikh Said Abry, amesema mradi huo wa ujenzi  wa majengo hayo mawili umegharimu kiasi cha Sh. Mil.703 na kuongeza kuwa mbali ya ujenzi huo pia wamefadhili vifaa tiba vyote vitakavyowekwa ndani ya majengo hayo na kuongeza kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia kuboresha sekta mbalimbali kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa muda mrefu hapa Nchini.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo