• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

JAMII YAMAHASISHWA KUZINGATIA LISHE BORA

Posted on: August 26th, 2020

Kila Familia na jamii inapaswa kufahamu kuhusiana na umuhimu wa lishe bora, kwani lishe bora ndio msingi wa Afya bora, familia imara na Taifa lenye nguvu.

Lishe bora maana yake ni mkusanyiko wa vyakula mbalimbali ambavyo kwa pamoja huimarisha na kuujenga mwili wa binadamu, vyakula hivi ni vile vyenye protini, mafuta na sukari, nafaka, vyakula jamii ya mikunde, mboga mboga na matunda.

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo Agosti 26, 2020 imeadhimisha siku ya lishe ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa aliyekuwa Mgeni rasmi, amewaongoza Wananchi kutoka pande zote za Halmashauri hiyo kushiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Top Top uliopo Kata ya Dunda ili kupata elimu ya masuala ya lishe kutoka kwa wataalam wa Afya na lishe bora waliotoka kwenye Taasisi zinazojihusisha na masuala ya lishe Wilayani Bagamoyo.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe, mratibu wa Lishe Wilaya Bi. Sophia Makame, amesema katika kipindi cha Mwaka 2019/2020 kitengo cha Lishe Wilaya kimefanikiwa kuongeza kiwango cha utoaji elimu ya lishe katika vituo vya kutolea huduma za Afya kutoka 88.4 Julai-Desemba 2019 hadi 116% Januari-Machi 2020, huku lishe ikiwekwa kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya maendeleo ya Kata kila robo ili elimu ya lishe ifike katika ngazi ya chini ya jamii na hii imesaidia kuongeza uelewa wa lishe bora kwa jamii kutoka wakina mama 6685-7360 huku watoto wanaotambulika kuwa na matatizo ya utapiamlo wakipatiwa matibabu na chakula dawa hivyo kuwasaidia kuondokana na tatizo hilo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa akizungumza katika maadhimisho hayo amesema amefarijika sana kuona kiwango cha elimu ya lishe bora kimeeleweka katika ngazi ya jamii na wakina mama kuweza kuandaa chakula bora kwa ajili ya familia zao na kingine kutengeneza kwa ajili ya kuuza na kujiongezea kipato huku akitumia fursa hiyo wanawake wanaonyonyesha kuzingatia unyonyeshaji wa watoto wao ili kuwajengea Afya bora na kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali ya utotoni.

“Takwimu zinaonesha kwamba 97% ya wanawake wananyonyesha watoto lakini hawazingatii maelekezo ya wataalam ya Afya katika kunyonyesha watoto huku 67% ya watoto wenye umri wa kuanzia miezi 06  hadi miaka 3 hawapati lishe bora hivyo kupelekea watoto hawa kupata utapiamlo, nawaasa wakinamama mzingatie kuwapa lishe bora watoto wenu na kuwapeleka kliniki kila mwezi ili kufatilia ukuaji wao na hali zao za lishe na wataalam wa Afya hakikisheni kila wakina mama wanapohudhuria kliniki mnatumia nafasi hiyo kuwapa elimu juu ya lishe bora kwa watoto wao ili tuwe na watoto wenye makuzi imara na tujenge Taifa imara la watu wenye lishe bora”. Amesema Mhe. Zainab

Takribani Miaka 20 sasa Tanzania imekua ikiadhimisha Siku ya Lishe na maboresho makubwa yamefanyika katika sekta ya lishe Nchini huku maadhimisho yam waka huu yakibebwa na kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kuwanyonyesha watoto kwa Afya bora na ulinzi wa Mazingira”



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo