• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

JIUNGENI NA CHF ILIYOBORESHWA MFAIDIKE: DC KAWAWA

Posted on: May 8th, 2019


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa ametoa rai kwa Wananchi wa Bagamoyo, hususani Wazee, kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa, ili iwasaidie kumudu huduma za matibabu pale wanapozihitaji.
Mhe. Zainab ameyasema hayo, mapema leo alipokuwa katika hafla maalum ya uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 2000 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Wazee wangu mliofika hapa leo na Wananchi wote wa Bagamoyo, ni vema wote tukumbuke kwamba maradhi huwa hayabishi hodi, na huja bila taarifa, litakuwa jambo la kheri yatakapotufikia tuwe tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha kila mmoja wetu amejiunga na mfuko wa Afya ya jamii kupitia mpango wa CHF iliyoboreshwa ambapo itakugharimu kiasi cha Shilingi 30,000/= tu, Mwaka mzima, kadi hii ya CHF iliyoboreshwa itakuwezesha kupata huduma bora za afya bure wewe na wategemezi wako 6, katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, Zahanati, Hospitali ya Wilaya na Hospitali kuu ya Mkoa” Amesema Mhe. Zainab
Nae mratibu wa dawati la Wazee, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Rajabu Mturuya katika taarifa yake aliyosoma mbele ya mgeni rasmi amesema, katika kipindi cha Januari – Machi 2019 Idara ya Afya kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii iliwapiga picha Wazee 2000 katika kata za Dunda, Magomeni, Nianjema, Kisutu, Kiromo, Zinga, Makurunge, Yombo na Fukayosi, na katika kipindi cha Oktoba – Desemba 2018 kata za Kerege na Mapinga jumla ya Wazee waliopigwa picha ni 349 ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuandaa vitambulisho vya matibabu ya wazee.
Hadi kufikia sasa Halmashauri ya Wilaya kupitia Idara ya Afya, imetoa jumla ya vitambulisho 750 kwa Wazee ambavyo wameanza kuvitumia kwa ajili ya kupata matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ndani ya Wilaya, hadi kufikia mwezi Juni 2019 Halmashauri inatarajia kutoa vitambulisho 2,000 kwa Wazee wote waliopigwa picha.
Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa amezindua bodi mpya ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambayo imeanza kazi tangu tarehe 13.03.2019 na inatarajiwa kutekeleza majukumu yake kwa muda wa miaka mitatu hadi tar. 13.03.2022.
Mhe. Zainab ameitaka bodi hiyo mpya kuhakikisha inasimamia vyema uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya, ili Wananchi wanufaike na uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya uliofanywa na Uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Chini ya Mhe. Rais, John Joseph Magufuli, iliyoleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya kwa kujenga vituo vipya vya Afya, Hospitali za Wilaya na utoaji wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri zote Nchini.
“Nendeni mkasimamie utoaji wa huduma bora za Afya, Hakikisheni Wazee na Wananchi wote kwa ujumla, wakifika katika vituo vya kutolea huduma wanapokelewa vizuri, hawasumbuliwi na wanapatiwa huduma stahiki kwani Sekta ya Afya ni Sekta yenye changamoto nyingi sana katika masuala ya utoaji huduma na muwe na ushirikiano ili sote kwa pamoja tuhakikishe huduma a Afya kwa Wananchi wa Bagamoyo zinaboreka.
Bodi mpya ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaundwa na wajumbe 6 na inaongozwa na Mwenyekiti Bi. Roswita F. Kasikila ambaye amemuahidi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na Wananchi wote wa Bagamoyo kuwa itafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo, kusimamia na kuhakikisha huduma za Afya ndani Halmashauri zinatolewa kwa ufanisi na weledi.
“Tutasimamia uanzishwaji wa dirisha la kuhudumia Wazee, tutashirikiana na Mkurugenzi, kupitia uongozi wa Idara ya Afya kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za Afya kinaanzisha dawati la kuhudumia Wazee, ili Wazee wasiendelee kupata usumbufu wanaoupata sasa wanapofika katika Vituo vya Afya kupata huduma” Amesema Bi. Roswita Kasikila.
Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ina wajibu wa Kuhakikisha jamii inapata huduma bora za Afya inazozimudu, na zinazoimarisha Afya zao, kujadili na kurekebisha mipango ya Afya na bajeti kisha kuwasilisha  kwa Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa, kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji kutoka kwa Timu za uendeshaji wa Huduma za Afya Halmashauri, kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na kukusanya rasilimali za kutosha kuendesha huduma za Afya za Halmasahuri na kusaidia timu za uendeshaji wa huduma za Afya ya Halmashauri katika kuiarisha rasilimali za Afya.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo