• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPAGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: November 21st, 2018


Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa robo ya kwanza ya Julai-Septemba ya Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Said Rajabu Ngatipura ilianza kwa kukagua kituo cha ukusanyaji mapato ya Mchanga kilichopo barabara ya Kiromo Chambezi katika Kata ya Kiromo.

Wakiwa katika kituo hiko wajumbe wa kamati hiyo wamepata taarifa ya ukusanyaji mapato kwa siku hadi mwezi, pia kusikiliza changamoto zinazokikabili kituo, huku wakiahidi kuzitafutia ufumbuzi zile zinazowezekana kutafutiwa ufumbuzi wa haraka, huku wakisisitiza uadilifu na uaminifu kwa wakusanyaji mapato katika kituo hiko.

Wajumbe pia wameitembelea na kuikagua barabara ya kiromo chambezi inayotumiwa zaidi na malori ya kubeba mchanga toka machimbo ya mchanga ya Kiromo chambezi, na kuona changamoto zinazoikabili barabara hiyo, suala ambalo wamelichukua ili kuona namna ya kulitaftia ufumbuzi na kumaliza kabisa changamoto zinazoikabili barabara hiyo kwa kushirikiana na wakala wa kusimamia ujenzi wa barabara za vijijini yaani TARURA.

Kamati pia imetembelea mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Matimbwa, kilichopo katika Kata ya Yombo na kukagua mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa fedha toka Serikali Kuu, kiasi cha Milioni 400 kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Kituo kinachotazamiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Novemba, 2018.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Matimbwa upo katika hatua za ukamilishaji, na mradi una jumla ya majengo makuu matatu ambayo ni Nyumba ya mtumishi, Jengo pacha linalojumuisha jengo la upasuaji na wodi ya wazazi, na jengo la tatu ni jengo la maabara.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Said Rajab Ngatipura akasisitiza wataalam wa Halmashauri kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya wakati uliopangwa na Serikali bila visingizio ili kutimiza adhma ya Serikali ya kuufadhili mradi huo.

Mradi mwingine uliotembelewa na kukaguliwa na kamati ni mradi wa Soko la Tandika, lililopo katika Kata ya Dunda, wakiwa katika eneo la mradi, kamati imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi inayoonesha mradi kukwama kuanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara kutohamia wala kuanza kufanya biashara katika soko hilo, kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki hususani soko kujaa maji wakati wa mvua.

Kamati imelichukua suala hilo kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wake, ili soko la tandika lianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Akihitimisha ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Said Rajabu Ngatipura aliwashukuru wasimamizi wa miradi katika sekta mbalimbali kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka watendaji wa Halmashauri kuipitia Mara kwa Mara miradi inayotekelezwa ili iweze kuleta tija kwa Wananchi.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo