• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KAMATI YA UELIMISHAJI JAMII YATAMBULISHWA BAGAMOYO

Posted on: February 15th, 2023

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mipango na mikakati mbalimbali ya serikali inatokana na jamaii kuelewa, kuhamasika na kushirikishwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo.

Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Bagamoyo, ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.

Alisema jamii inahitaji kupata elimu juu ya jambo husika ili waweze kushiriki kikamilifu katka mambo mbalimbali yanayoandaliwa na serikali na kwa kutambua hilo serikali imeweza kuandaa namna ya kuwashirikisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha kupitia kamati hiyo.

Ameitaka Kamati hiyo itakapopata elimu juu ya kile wanachotakiwa kwenda kukifanya wakafanye kwa utaalamu waa hali ya juu kwa kuwafikia makundi mbalimbaali katika jamii.

Aliwakumbusha kuwa, kazi yao kubwa ni kwenda akutoa elimu, kuhamasisha na kuwashirikisha kuhusu magonjwa ya mlipuko ili kila mmoja awe na uelewa ulio sahihi hali itakayosaidia kwa serikali kutotumia nguvu katika kuhamasisha chanjo zaa magonjwa ya mlipuko.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu,  amesema kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, imeundwa ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambapo wananchi wanapaswa kupata elimu sahihi kuhusu magonjwa hayo ili waweze kujilinda na kujitibu.

Alisema lengo la mkutano huo ni kutambulisha kamati ambayo itashiriki katika kutoa elimu, kuhamasisha, na kushirikisha jamii ili waweze kuelewa madhara ya magonjwa ya mlipuko.

Nae Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo amesema wanatarajia kupata mafanikio katika Kamati hiyo iliyotambulishwa kwakuwa imeshirikisha makundi mbalimbali ya kijamii.

Alisema mara kadhaa serikali inapotaka jambo la kijamii liwafikie wananchi hutumia makundi mbalimbali ya kijamii ili kurahisisha ufikishaji wa taarifa kutokana na kamati husika kukubalika katika jamii kwani miongoni mwao wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa viongozi wa dini, serikali na asasi za kiraia.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mafanikio katika kutoa elimu kuhusu magonjwa ya mlipuko ni jambo kwakuwa tutakuwa tumemsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amekuwa akihakikisha wananchi wake wanakuwa salama dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Alisema Rais Samia ni mpenda maendeleo hivyo anapenda wananchi wake wawe na afya njema ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo wenyewe na taifa kwa ujumla.

Aidha, amewashukuru Wizara ya Afya kitengo cha Elimu ya afya kwa uma kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kuchagua mkoa wa Pwani kuwa miongoni mwa mikoa inayostahili kupata kamati hiyo ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko.

Mkutano huo wa kutambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, umeandaliwaa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Shirika la Afya duniani W.H.O. 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023.  katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.


Afisa Mipango wa huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya afya, Bahati Mwailafu, akizungumza na washiriki wakati wa Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.


Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma wilaya ya Bagamoyo, Jeni Mcharo, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi mara baada ya kumalizika kwa   Mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Ushirikishaji na Uelimishaji jamii, kuhusu magonjwa ya mlipuko uliofanyika leo Februari 15, 2023. katika Ukumbi wa Chuo cha unesi Bagamoyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo