• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KITUO CHA AFYA KEREGE KUANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI HIVI KARIBUNI

Posted on: May 25th, 2018


Kituo kipya cha Afya Kerege kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali kuu mapema mwishoni mwa mwaka jana (2017) kitaanza rasmi kutoa huduma za upasuji hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu ameyasema hayo leo jioni ya leo tarehe 25. 05. 2018 alipokuwa akizungumza na wageni mbalimbali aliowaalika futari maalum aliyowaandalia wadau hao kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imejenga kituo bora kabisa cha Afya nchini baada ya kufadhiliwa jumla ya Tshs.Milioni 500 na Serikali kuu na kujenga kituo hicho cha Afya Kerege kwa kutumia “Force account” na tayari kimeanza kutoa huduma za kuzalisha wakina Mama na huduma nyingine muhimu za kiafya na huduma ya upasuaji itaanza kutolewa mara tu baada ya kukamilika kwa ununuzi wa vifaa tiba katika Kituo hicho cha Afya.

Ujenzi wa kituo cha afya kerege ulianza tarehe 20/10/2017 na lengo kuu la mradi likiwa ni kuboresha vituo vya afya nchini na kuwa na vituo vya afya vyenye ufanisi.

Bi. Latu anasema hadi sasa Kituo cha Afya Kerege kimejenga na kukamilisha Jengo la upasuaji, Jengo la wazazi, Nyumba ya mtumishi, Jengo la maabara, Jengo kwa ajili ya mfumo wa umeme na jenereta, Mashimo mawili ya kuvunia maji, Minara miwili ya kuvunia maji yenye vyoo na stoo chini, Kichomea taka huku Jengo la kufulia nguo na Jengo la kuhifadhia maiti yakiwa katika hatua za ukamilishaji.

Akaongeza, Mradi ulikadiriwa kugharimu jumla ya Tsh 544, 000,000.00 ambapo kiasi cha Tshs 500, 000,000.00 ilipokelewa kutoka OR-TAMISEMI na kiasi cha Tshs. 44,000,000 ni mchango wa Halmashauri.

Hadi sasa kiasi cha Tsh 478, 000,000.00 zimetumika ambapo kiasi cha Tshs 460, 000,000.00 kimetumika katika ujenzi na Tshs 18, 000,000 kimetumika katika shughuli za usimamizi wa mradi.

Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kutolewa kwa huduma za Afya kwa ufanisi zaidi zikiwemo huduma za dharura na kufanya upasuaji hasa kwa akina Mama wajawazito wakati wa kujifungua lakini pia upasuaji wa kawaida kwa wagonjwa wengine watakaohitajika kupata huduma hiyo.

Kituo cha Afya Kerege kina uwezo wa kutoa huduma kwa Jumla ya wananchi 7,114 wa Kata ya Kerege lakini kinatarajiwa pia kuhudumia wakazi wa Kata jirani.

Akaongeza kuwa baada ya kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kerege kwa ufanisi mkubwa, Serikali na wadau wengine wa maendeleo wamesema wapo tayari kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambayo ni Ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa ya mabasi na Soko jipya la kisasa la samaki katika pwani ya Bagamoyo.

Wadau mbalimbali wa Halmashauri wapatao 200, ikiwa ni pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, wakuu wa Idara, Viongozi wa jumuiya ya kuendeleza na kutunza Amani, Viongozi wa dini, Viongozi wa taasisi za kifedha, Viongozi wa taasisi zingine za Serikali ndani ya Halmashauri na asasi zisizo za Kiserikali, Viongozi wa Wanawake, Wazee na watu wenye ulemavu, na Watumishi wa Halmashauri walipata fursa ya kuketi pamoja katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na kufuturu pamoja.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo