• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KIWANDA CHA BAGAMOYO SUGAR KUANZA UZALISHAJI JUNI 2021

Posted on: August 16th, 2018



Kiwanda cha uzalishaji Sukari cha Bagamoyo Sugar, kinatarajia kuanza uzalishaji wa Sukari mnamo mnamo Juni 2021.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa mradi huo Bw. Muharami Muharami, mapema leo mchana mara baada ya kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani kufika kukagua uendelevu wa mradi huo unaotekelezwa katika kitongoji cha Razaba kilichopo Kata ya Makurunge Wilayani Bagamoyo.
Mradi huo wa ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji Sukari cha Bagamoyo Sugar upo katika hatua za awali za upandaji mbegu za miwa yaani “nursery” ambazo zimepandwa katika shamba lenye ukubwa wa hekta 8 ambazo zipo kwenye majaribio ya kutafuta mbegu moja bora itakayofaa kulimwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 10,000 kwa kutumia mfumo wa kilimo cha umwagiliaji cha matone almaarufu kama “drip irrigation”
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Eng. Evarist Ndikilo akizungumza katika ziara hiyo ya ukaguzi wa mradi huo wa Shamba la miwa na ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji Sukari cha Bagamoyo Sugar amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kutekeleza Sera ya Tanzania ya Viwanda, ilitoa eneo hilo kwa kampuni ya Bagamoyo Sugar ambayo ni kampuni tanzu ya Bakhresa group of companies, iliyoomba kutekeleza mradi huo katika eneo hilo.
Mhe. Ndikilo anaongeza, “Serikali baada ya kuchoshwa na uhaba wa sukari Nchini, iliamua kutoa eneo hilo kwa mwekezaji wa ndani, ili atekeleze mradi huo ambao uwekezaji wake utatumia jumla ya dola Milioni 75 na kiwanda hicho kipya cha sukari kinatarajia kuzalisha sukari kati ya tani 30,000 hadi 70,000 za sukari kwa Mwaka”.
Akatumia fursa hiyo pia kuwahamasisha Wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho katika eneo hilo kulima miwa yaani “out growers” na kuja kuuza kiwandani hapo mara uzalishaji wa Sukari katika kiwanda hicho cha Bagamoyo Sugar utakapoanza ili waweze kunufaika na mradi huo lakini pia kujikwamua kiuchumi.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mhe. Ramadhan Maneno, akiwa katika ziara hiyo amekemea tabia ya baadhi ya Wananchi kuvamia maeneo ya Wawekezaji na kuanzisha makazi ya kudumu na wengine kuingiza mifugo katika maeneo ya mashamba ya wawekezaji hali inayopelekea migongano isiyo ya lazima baina ya Wawekezaji na Wananchi.
Mhe. Maneno pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye tija hususani mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kerege ambao umekamilika na umeanza kutoa huduma ambapo hadi sasa Wakina mama 127 wameshajifungua katika Kituo hicho kipya cha Afya.
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani leo imemaliza ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa huo na wakiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wametembelea jumla ya miradi minne ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kerege kilichopo Kata ya Kerege, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo eneo la Mbegani, Ujenzi wa tanki la Maji lenye ujazo wa Lita Milioni sita (6) unaotekelezwa na DAWASA katika Kata ya Magomeni, pamoja na mradi wa shamba la miwa na ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo Sugar katika kitongoji cha RAZABA kilichopo Kata ya Makurunge.





Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo