• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KLINIKI YA SIKOSELI YAANZISHWA HOSPITALI YA WILAYA YA BAGAMOYO

Posted on: September 14th, 2020

Ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu Serikali kuzindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa sikoseli mnamo Juni 19,2020 huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiagiza kuanzishwa kwa kliniki maalumu za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuhakikisha watu wengi hasa watoto wanafikiwa, Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS) program ya selimundu wakiongozwa na Dkt. Agnes Jonathan, leo wameanza rasmi utoaji huduma katika kliniki maalum kwa wagonjwa wa sikoseli katika Hospitali y Wilaya ya Bagamoyo ili kusaidia wakazi wa Bagamoyo kupata huduma ya utambuzi ya ugonjwa wa sikoseli kwa ukaribu zaidi.

Uzinduzi wa utoaji huduma hizo katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo umefanyika leo Septemba 14, 2020, hospitalini hapo ambapo Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Mohamed Farah pamoja na kuwashukuru wataalam hao waliofika kutoa huduma ya kliniki ya sikoseli, amesema hii ni fursa adhimu kwa Wananchi na wakazi wa Bagamoyo kufika Hospitalini hapo ili kupata huduma hiyo na kwamba baada ya uzinduzi huo kliniki itakuwa wazi kwa wagonjwa wa sikoseli kila siku ya jumatatu kuanzia leo na jumatatu zijazo.

Mratibu wa program ya sikoseli toka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) Dkt. Agnes Jonathan aliyeongoza timu ya wataalam kutoka Muhimbili waliofika Bagamoyo kuendesha kliniki kwa wagonjwa wa Sikoseli ametoa mafunzo maalum kwa wazazi wenye watoto walio na tatizo la sikoseli juu ya namna ya kuutambua ugonjwa huo, dalili zake, athari na viashiria vya hatari ambavyo mzazi anapoviona amuwahishe mtoto wake Hospitalini kwa matibabu zaidi bila kungoja siku ya kliniki.

“Jamii imekua na dhana potofu juu ya ugonjwa wa sikoseli, leo ni vema mkafahamu kwamba ugonjwa huu ni wa kuithi pale wenza wawili wenye vinasaba vya ugonjwa huu wanapopata mtoto, mtoto huyo anaweza kupata ugonjwa wa sikoseli ambao mara nyingi hutambulika mara mtoto anapofikisha umri wa miezi 6, kwa kupata tatizo la upungufu wa damu mara kwa mara, lakini ni vema zaidi mkitambua kuwa ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wa Afya ikiwa ni pamoja na unywaji wa maji mengi walau lita 3 kila siku, kuzingatia lishe bora na kuhudhuria kliniki ambayo sasa kwa Bagamoyo huduma imesogezwa kwani kliniki hiyo itakuwa inafanyika kila siku ya Jumatatu katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo” Amesema Dkt. Agnes

Nae. Bi. Arafa Said Mwanzilishi na Rais wa Asasi isiyo ya Kiserikali iitwayo Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania ambaye ameongozana na wataalam hao katika uzinduzi huo amewatia moyo wazazi wenye watoto wenye tatizo la selimundu kwani pamoja na yeye kuishi na ugonjwa wa sikoseli lakini kwa kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Afya ameweza kuendelea na maisha yake hata kufikia hatua ya kuwa na familia.

Mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa Sikoseli, ulizinduliwa rasmi Juni 19,2020 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ukiwa na kauli mbiu inayosema “Huduma Bora kwa Kila Mhitaji; Chukua hatua, panua wigo.” na katika kutekeleza kauli mbiu hiyo, Wataalam toka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS) wameanza kuzifikia Halmashauri za Wilaya na kuanzisha kliniki za wagonjwa wa sikoseli huku Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni moja ya Halmashauri za mwanzoni kunufaika na utaratibu huo.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo