• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

RAS PWANI AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA NGUVU KATIKA UKUSANYAJI MAPATO

Posted on: September 12th, 2018


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Theresia Mmbando, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, katika kikao maalumu cha kujitambulisha kwa Watumishi, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mapema jana asubuhi.

Bi. Mmbando amesisitiza kuwa kipaumbele cha sasa cha Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli ni kuhakikisha Serikali inakusanya mapato kwa nguvu na kwa ufanisi.

“Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia malengo mliyojiwekea kama Halmashauri katika kukusanya mapato ya ndani katika Mwaka huu wa fedha, fuatilieni ufujaji wa mapato katika vyanzo vyenu na hakikisheni mnaziba mianya yote ya ufujaji kwa kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kujihusisha na ufujaji wa mapato” Anasema Bi. Mmbando.

Anaongeza kusema kuwa, ili Halmashauri ipate uwezo wa kujiendesha vizuri, ni lazima ukusanyaji wa mapato ya ndani uwe ni wa uhakika, hivyo kuwataka Watumishi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, kukusanya mapato ya Halmashauri kwa nguvu zote.

Bi. Mmbando pia ametumia fursa hiyo kuelezea vipaumbele vya Serikali na kusisitiza uwajibikaji unaozingatia weledi kwa watumishi, bila kusubiri kusukumwa na viongozi ili kuhakikisha wanamaliza kero na malalamiko ya Wananchi kwa wakati.

Kupitia kikao hicho Bi. Mmbando pia amesikiliza kero wanazokutana nazo watumishi wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya ila siku, kero ambazo zilitolewa ufafanuzi wa kina na Afisa utumishi wa Halmashauri Bw. George Mwalukasa.

Kero zilizowasilishwa na watumishi ni pamoja na ucheleweshwaji wa kupandishwa madaraja, kutolipwa stahili za posho za likizo, kutopitishiwa barua za uhamisho na wakuu wao wa Idara wanapohitaji kuomba uhamisho, kucheleweshwa kwa malipo ya mishahara ya watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani, kuchelewa kwa malipo ya fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya, upungufu mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya unaopelekea utoaji hafifu wa huduma katika Hospitali ya Wilaya na watumishi wanaohitaji kubadilishiwa muundo wa utumishi.

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi. Theresia Mmbando yupo katika ziara maalumu ya kujitambulisha kwa Watumishi wa Halmashauri za Mkoa wa Pwani, baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani akitokea Mkoa wa Dar Es Salaam.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo