• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MAADHIMISHO MIAKA 61 YA UHURU YAFANYA WILAYANI BAGAMOYO..

Posted on: December 9th, 2022


Madhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara Wilayani Bagamoyo ambapo katika maadhimisho hayo kumetolewa mada mbalimbali kuhusu Uhuru wa Tanzania bara pamoja na

Taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wilaya ya Bagamoyo kueleza Maendeleo na Mafanikio waliyoyapata  toka mwaka 1961 mpaka hivi Sasa


Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Lugoba mbele ya mgeni rasmi,Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Bi. Kasilda Jeremiah Mgeni. Kulifanyika shughuli mbalimbali kama michezo ya mpira wa miguu,upandaji miti,usafi wa mazingira na kongamo lililohusisha wananchi wote katika upokeaji wa mafanikio yaliyofikiwa na Serikali katika kuwahudumia wananchi na wananchi walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa mafanikio ya Serikali katika sekta mbalimbali.


Katika kongamano hilo wataalam katika sekta mbalimbali walipata fursa ya kutoa maada mbalimbali kisekta na jinsi mafanikio yalivyopatikana ndani ya miaka 61 ya uhuru, maada zilizowasilishwa ni Siasa na Utawala Bora,Ufanisi katika Huduma za Jamii(Afya, Maji, Elimu na Nishati, Hali ya Uchumi, Kilimo,Viwanda, Biashara na Miundombinu.


Aidha wananchi walipata fursa ya kutoa maoni mbalimbali kuhusiana na mafanikio yaliyofikiwa ndani ya miaka 61 sanjari na kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni:”Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo yetu.”

“Serikali yetu imepiga hatua kubwa katika suala la Utawala bora,kwani mwanzo maelekezo yalitoka juu kushuka chini lakini kwa sasa wananchi tunaweza kutoa mahitaji yetu kutoka chini kwenda juu kutokana na vipaumbele vyetu na yakafanyiwa kazi hii ni hatua kubwa kiutawala ndani ya miaka 61 ya Uhuru wetu.” Shekh Nassoro alisema.


Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya, *Mhe Kasilda Mgeni* aliwapongeza watoa mada wote katika kongamano hilo kwa kuweza kuyabainisha mafanikio ya Serikali kwa kina kisekta ndani miaka 61 ya uhuru wa Taifa la Tanzania na kuwataka washiriki wote kuwa mabalozi katika kuyasema mafanikio hayo hadharani kwani ndiyo uhalisia uliopo.

“Ndugu washiriki niwapongeze wote kwa jinsi mlivyoweza kuyasema kwa kina mafanikio ya Serikali katika nyanja mbalimbali za maisha,pia niwapongeze viongozi wote waliowahi kuliongoza Taifa hili kuanzia muasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin William Mkapa, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali walizozifanya na zinazoendelea kufanyika katika kuliletea matokeo chanya Taifa hili.” Mgeni Rasmi alisema.


Pia baadhi ya Viongozi mbalimbali wa kidini wakitoa wasio wao Kwa wananchi wa Bagamoyo na Tanzania kiujumla kuendelea kulinda Amani ya Tanzania.


Wilaya ya Bagamoyo imefanya zoezi la upandaji wa miti Pamoja na kufanya usafi maeneo mbalimbali katika Wilaya, yote ni kuendelea kuenzi Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


"Amani ná Umoja ni Nguzo ya Maendeleo yetu".

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo