• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MAADHIMISHO YA SIKU YA ELIMU BAGAMOYO YAFANA

Posted on: June 6th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeadhimisha siku ya Elimu Kiwilaya ambapo maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa Taasisi, Shule na Wadau wengine wa elimu, kutafakari maendeleo ya elimu na changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu.

Maadhimisho hayo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo yamefanyika jana tarehe 05/06/2018 na kuhudhuriwa na Walimu, Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo, Taasisi mbalimbali za elimu, Wadau wa Elimu, Taasisi za kifedha, Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri, Wakuu wa Idara za Halmashauri na Wananchi.

Kauli mbiu iliyopamba kilele cha maadhimisho ya Siku ya Elimu kwa mwaka 2018 ilikuwa ni “UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KWA ELIMU BORA KWA WATU WOTE” huku mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Alhaj Majid Mwanga ambaye aliwakilishwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya ADEM Ndg. Alphonce J. Amuli.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mgeni Rasmi Ndg. Alphonce Amuli amesema, Ili kuboresha kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari, ni lazima Walimu, Wazazi na wadau wengine wa elimu wawe na ushirikiano mkubwa kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya Mwanafunzi mmoja mmoja kwa karibu, na Mwanafunzi anaporudi nyumbani, Mzazi ahakikishe anamsimamia na kumkumbusha mtoto kujisomea, kufanya kazi alizopewa shuleni ‘home work’ na kuhakikisha anamfatilia kama mtoto kweli anafika shuleni kila siku.

Akaongeza “Serikali imeboresha na kuongeza miundombinu katika Sekta ya Elimu kama vyumba vya madarasa na madawati, lakini pia inahakikisha inatekeleza dhana ya ‘Elimu Bure’ kwa vitendo kwani kila mwezi imekuwa ikitoa fedha zinazopelekwa moja kwa moja Shuleni ili kuhakikisha Wanafunzi kote nchini kuanzia Darasa la kwanza hadi kidato cha nne wanapata Elimu Bure”

Akasisitiza, “Fedha zinazotolewa na Serikali ili kuboresha Sekta ya Elimu nchini, zisimamiwe vizuri hasa fedha za Elimu Bure, Walimu wakuu wa Shule wahakikishe fedha hizo zinasimamiwa vizuri na zinafanya kazi iliyokusudiwa na Serikali ili kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha Elimu ya Msingi nchini, inatolewa bure na kila mtoto mwenye umri wa kuanza shule apelekwe Shule ili kutimiza adha ya Serikali ya kutokomeza ujinga nchini.

“Ni lazima tujiulize, ni aina gani ya elimu tunahitaji kuwapatia watoto wetu hasa wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya tano, imeshikilia na inatekeleza kauli mbiu yake ya Tanzania ya Viwanda, Je elimu tunayowapatia watoto wetu huko mashuleni inawandaa kwenda na kasi ya Tanzania ya viwanda? Watoto wanapatiwa stadi za ufundi, wanafundishwa kuwa wabunifu na kusisitizwa kujikita katika masomo ya sayansi ya uzalishaji lakini pia kuweka mkazo katika taaluma zitakazowasaidia kujiaijiri na kuajiriwa kwenye Tanzania mpya ya viwanda?” Anasema Ndg. Amuli.

Mhe. Mgeni rasmi akaongeza, ni vyema Walimu wakawekeza pia katika uboreshaji wa shughuli za Sanaa na michezo kwa Wanafunzi wao kwani Sanaa na Michezo ni ajira, hujenga afya na inasaidaia kutunza, kuhifadhi na kurithisha utamaduni wetu wa Mtanzania kwa watoto wetu kupitia Sanaa mbalimbali za maonesho.

Akizungumzia mdondoko wa Wanafunzi unachangiwaa na mimba pia utoro, Ndg. Amuli anawanasihi Wazazi, Walimu, Wanafunzi na Wadau mbalimbali wa Elimu kuwa, suala hili linahitaji ushirikiano mkubwa baina yao kulidhibiti kila mmoja kwa nafasi yake lakini Mwanafunzi ahakikishe anazingatia masomo yake, asome kwa bidii huku akijitahidi kujiepusha na vishawishi vya kimapenzi vinavyoweza kupelekea akatishe masomo yake kwa kupata ujauzito.

Mgeni rasmi Ndg. Alphonce Amuli kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Alhaj Majid Mwanga, pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa Halmashauri yake kuibuka kidedea na kushika nafasi ya kwanza Kitaifa katika mitihani ya kidato cha nne iloyofanyika Novemba mwaka jana 2017.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Ndg. Peter Fussi amesema katika kuboresha sekta ya elimu Kiwilaya, Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wanaendelea na ujenzi wa vyumba 74 vya madarasa katika  Kata za Halmashauri, umaliziaji wa maabara 2 katika Shule ya Sekondari Kingani, Ujenzi wa bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Dunda, ujenzi wa jengo la utawala Shule ya Sekondari Kerege na Hassanal Damji,na kwamba kukamilika kwa miradi hii na kuanza kutumika kutasaidia kufanya mazingira ya kusomea na kufundishia kuwa bora na hivyo kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi.

Maadhimisho ya siku ya elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagomoyo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Majengo ambapo yalitanguliwa na maandamano ya Walimu, Wanafunzi na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri na yalianzia katika Ofisi za Halmashauri.

 Pia maadhimisho hayo yalipambwa kwa maonesho ya huduma za elimu toka taasisi mbalimbali za elimu zinazofanya kazi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na taasisi za kifedha na utoaji zawadi kwa Shule zilizofanya vizuri kwa upande wa usafi wa mazingira wa Shule zao, lakini pia utoaji zawadi kwa Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la nne, darasa la saba, mtihani wa upimaji wa kidato cha pili na mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2017.





Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo