• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI JUKUMU LETU SOTE: DC BAGAMOYO

Posted on: October 2nd, 2020

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Farah Mohamed, alipomwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Zainab Kawawa katika uzinduzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali iitwayo Youth and Community Rehabilitation (YCR) inayojishughulisha utoaji elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na uhamsishaji waraibu wa dawa za kulevya kujiunga na matibabu ya Methadone.


Matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa ni tatizo na janga kubwa kwa Vijana waishio katika ukanda huu wa Pwani ya Bahari ya Hindi kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo kibiashara katika eneo hili hivyo uingiaji na matumizi ya dawa za kulevya unarahisishwa na mwingiliano wa watu na shughuli zinazofanyika katika ukanda huu.

“Ni wajibu wa kila mwanajamii kujitahidi kufuatilia, kusimamia na kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya katika jamii yetu ili kuwasaidia Vijana wetu na kurejesha nguvu kazi ya Taifa letu .kwani Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa, na Taifa lisilo na Vijana wenye Afya njema, Taifa hilo haliwezi kuendelea kiuchum”. AMmesema Ndg. Farah.

Anaongeza, Asasi ya YCR imekuja kutusaidia wanaBagamoyo kuwaibua Vijana wetu ambao wameshapata madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, ili kuwaelimisha na kuwamasisha kujiunga na matibabu ya Methadone, ni wajibu wetu kama jamii kuwapa ushirikiano mkubwa, katia utambuzi wa Vijana wetu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya ili wapatiwe elimu kisha wapelekwe kupata matibabu ya methadone, Matibabu haya ni salama na ni bure hivyo tutoe ushirikiano mkubwa kwa  YCR Vijana wetu wapate tiba, wawe na Afya njema na warudi katika ujenzi wa Taifa letu”

Dkt. Norman Sabuni kutoka Taasisi ya kupambana na dawa za Kulevya Nchini, ambaye alihudhuria katika uzinduzi wa Asasi hiyo ameelezea hali ya matumizi ya dawa za kulevya Nchini, na kutanabaisha kuwa, tatizo hilo bado ni kubwa Nchini na linapelekea vifo, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kwenye jamii, Kupungua kwa nguvu kazi ya jamii, kuweka hatarini usalama wa jamii hasa watoto kwa utupaji hovyo wa mabomba ya kudungia sindano yanayotumiwa na waraibu wa dawa za kulevya, na kuongeza gharama za huduma za Afya kwa Serikali kulazimika kujenga na kuanzisha kliniki za Methadone na matibabu yake Nchini na katoa rai kwa wanajamii kutoa ushirikiano kwa asasi ya YCR ili kusaidia waraibu kwenda kwenye matibabu ya Methadone ili kuirejesha jamii ya waraibu katika hali ya kawaida na kuanza kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Husna Kipilipili ni mratibu wa Kliniki ya Methadone Wilaya ya Bagamoyo na ameelezea namna Vijana waraibu wa dawa za kulevya Wilayani hapa wamepokea huduma hiyo ya kunywa dawa za Methadone na akaongeza kwamba hadi sasa jumla ya Vijana 123 wameshaanza program hiyo na wanaendelea vizuri sana, huku wengine 40 wakiwa katika uangalizi na kupatiwa elimu kwanza kabla ya kuingizwa katika program hiyo ya kunywa dawa za Methadone maana ni lazima mraibu apate elimu ya kutosha kwanza kisha aridhie mwenyewe  kuanza matibabu ya Methadone.

Nae Ndg. Alex Chitawala ni Meneja wa Vituo vya YCR Nchini, ambapo ameelezea kuwa hadi sasa Asasi hiyo ina Vituo vya uelimishaji na uhamasishaji Waraibu wa dawa za kulevya kujiunga kwenye matibabu ya Methadone katika Mkoa wa Pwani, Arusha na Dodoma.

“Tunatarajia kupanua wigo wa utoaji huduma kwa kuufikia Mkoa wa Arusha, Ofisi zetu za Arusha zitaanza kufanya kazi wiki ijayo na Lengo hasa la program hii ni kuhakiksha walengwa ambao wanapaswa kuingia katika matibabu ya tiba ya methadone, wanapata huduma iliyo bora na inayostahili kutokana na uzoefu ambao sisi kama YCR tumekua nao” Amesema Ndg. Chitawala

Hapa Bagamoyo Huduma katika Ofisi za YCR zimeanza kutolewa rasmi leo Oktoba 02 Oktoba, 2020 na tunamshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kuja kuzindua shughuli zetu hizi ambazo zitakua zikifanyika katika Halmashauri yetu ya Bagamoyo katika eneo la caravan serai

Akitoa wito kwa wana jamii ya Bagamoyo Ndg. Chitawala amesema, tatizo la matumizi ya dawa za kulevya linatiba, kwahiyo jamii tuungane kupitia kituo hiki, tupo tayari kuwafikia popote walipo watupe ushirikiano ili tuweze kutoa huduma bora kwa waraibu wa dawa za kulevya waliopo katika jamii kwa kuwasaidia kupata matibabu ya methadone na kuondokana kabisa na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya, tusiwanyanyapae na kuwaona hawafai ama kwa kuwaona wahalifu maana mtazamo huo hausaidii kuondoa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya katika jamii lakini tukiwapenda na kuwasaidia nina hakika lengo la Bagamoyo bila dawa za kulevya tutalifikia kwa haraka na kwa pamoja.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo