• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MAPINGA YAIBUKA KIDEDEA USAFI WA MAZINGIRA

Posted on: September 21st, 2018


Kata ya Mapinga imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Usafi wa mazingira yaliyoendeshwa chini ya Idara ya Afya na usafi wa mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampeni ya usichukulie poa nyumba ni choo, yaliendeshwa katika Kata 5 za Halmashauri ya Wilaya ya bagamoyo, ambazo ni kata ya Mapinga, Kerege, Yombo, Magomeni na Dunda.

Akizunguzumzia namna mashindano hayo yalivyoendeshwa, Afisa Afya Wilaya ya Bagamoyo, Bi Anna Chiganga amesema ili kumpata mshindi walizingatia vigezo vya uwepo wa dampo katika kata, uwasilishaji wa taarifa za usafi wa mazingira kutoka Kata kuja Wilayani, Idadi ya nyumba bora zenye vyoo bora vya kudumu katika Kaya ndani ya Kata, namna sharia ndogo za usafi wa mazingira zinavyotekelezwa katika Kata na mwisho ni miundo mbinu ya usafi kama mifereji ya kupitisha maji taka nk.

“Ni dhamira yetu kuuona mji wa bagamoyo ukiwa safi na Wananchi wakipewa elimu ya kutosha juu ya kuishi katika mazingira safi hususani kuwa na choo bora na sehemu ya kunawa mikono yenye chombo kinachotiririsha maji, hii itasaidia sana kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu, homa na maradhi mengineyo yatokanayo na kuishi katika mazingira machafu lakini pia kuwa na Bagamoyo safi” Anasema Bi. Chiganga.

Anaongeza kuwa Lengo la mashindano haya ya usafi ya Kata, ni kuamsha ari ya Wananchi kufanya usafi bila kusukumwa na kufanya usafi kuwai tabia huku akibainisha kwamba kwa mwaka ujao wamejipanga kufanya mashindano hayo katika Kata zote 11 za Halmashauri.

Bi. Chiganga anasema, kupitia mashindano hayo ya usafi wamebaini changamoto kadhaa ikiwemo ya Wananchi kudhani jukumu la kufanya usafi wa amzingira si lao bali ni la Serikali, hususani kuwajengea vyoo bora, lakini wamejipanga kuhakikisha Wananchi hawa wanajengewa uelewa kuhusu masuala ya usafi na baada ya hapo wataanza kuchukua hatua kwa wote wataoendelea kukaidi kufanya usafi wa mazingira uanayowazunguka na kugoma kujenga choo bora kwa kuwapiga faini na kuwapeleka katika mabaraza ya Kata.

Ushindi wa kwanza katika mashindano hayo ya usafi ya Kata, ulichukuliwa na Kata ya Mapinga ambao wamezawadiwa toroli 2, Viatu vya kufanyia usafi “boots” jozi 4, Fagio laini 2, Fagio ngumu 2 na cheti cha ushiriki, huku nafasi ya pili ikishikwa na Kata ya Dunda, ikifuatiwa na Kata za Magomeni nafasi ya 3, Kerege nafasi ya 4 na Yombo kushika nafasi ya 5.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo