• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

ULINZI WA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE - DC BAGAMOYO

Posted on: June 15th, 2018


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Alhaj Majid A. Mwanga amewataka wazazi na walezi Wilayani humo kujenga tabia ya kuwalinda wototo na kuwafundisha watoto jinsi ya kujilinda ili kupunguza kama si kumaliza kabisa matukio ya ukatili kwa watoto yanayoendelea nchini hivi sasa.


Mhe. Mwanga ameyasema hayo jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayofanyika kila mwaka na kwa Wilaya ya Bagamoyo maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Majengo iliyopo Kata ya Magomeni ambapo yalipambwa pia na maonesho toka kwa taasisi za serikali na asasi zisizo za Kiserikali zinazotoa huduma mbalimbali kwa watoto.


“Watoto wana haki ya kupata elimu, kulindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia, kupendwa na kuthaminiwa, wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakikisha watoto wao wanaishi katika mazingira salama wakati wote hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu za Eid, mtoto atakayepotea tutahakikisha tunakukamata wewe mzazi/mlezi kwa kushindwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto wako, kazi ya ulezi itakuwa imekushinda” Amesema Mwanga


Anaongeza, Ni marufuku watoto kwenda disko, watoto kazi yao ni kusoma sio kwenda disko, nachukua nafasi hii kupiga marufuku disko toto katika Wilaya ya Bagamoyo, atakayekusanya watoto mahali kwa minajili ya kutoa burudani ya disko toto tutamshughulikia”


Akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi hellen Kisanji akizungumzia hali ya watoto Wilayani humo anasema kwa sasa Halmashauri inashirikiana na wadau mbalimbali na asasi zisizo za Kiserikali kutoa elimu ya jinsi ya kuepuka ukatili wa kijinsia kwa watoto na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa vituo vya kulelea watoto Wilayani humo kuhakikisha wanaendesha vituo vyao na kutoa huduma hiyo kwa watoto kwa kufuata taratibu miongozo na sheria zilizowekwa na Serikali.


Kwa upande wa Afya, Bi. Kisanji anasema Kwa mwaka 2017 Wilaya ilitarajia kutoa chanjo kwa watoto 12,342 ikiwa ni lengo la utoaji matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto 9,550 wenye umri chini ya mwaka mmoja, lengo ambalo lilifanikiwa kwani jumla ya watoto 11,342 walipata chanjo yam atone ya vitamin A, sawa na asilimia 90, na watoto 8545 walipata dawa za minyoo sawa na asilimia 89 ya lengo, na kwa mwaka 2018 Halmashauri inatarajia kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuwafikia watoto 12,342 kwa kuwapatia matone ya Vitamin A na watoto 10,708 watapewa dawa za minyoo na zoezi la utoaji wa chanjo hizi kwa mwaka 2018 tayari limeanza tangu tarehe 01/06/2018 katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Wilayani Bagamoyo.


Nae mmoja wa wadau wa masuala ya watoto Wilayani Bagamoyo ambae pia ni mmiliki wa kituo cha Afya ya Mama na mtoto kiitwacho FACGBF Nursing and Maternity home, Bi. Asnath Mchopa amesema ni vyema sasa jamii ikashirikiana kwa nguvu zote kupiga vita ukatili wa kijinsia kwa watoto na kuhakikisha wanakomesha tatizo la mimba za utotoni kwani tatizo hilo linarudisha nyuma ndoto za mtoto ama kuzikatisha kabisa.


Maadhimisho hayo pia yalipambwa kwa utoaji zawadi na misaada kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima na walio kwenye mazingira hatarishi na misaada kwa baadhi ya wazazi na walezi wasio na uwezo na wenye changamoto kubwa za kiuchumi zinazopelekea kushindwa kuwapa mahitaji mahumu watoto wao na vitambulisho 200 vya bima za Afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.


Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka Afrika na duniani kote na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali Wilayani hapa zikiwemo Hope for Young Girls, CAMFED, Compassion, Sasamani Village, Room to read na nyinginyezo zimekuwa zinajitolea kuhakikisha wanapigania haki za watoto na kutoa elimu zinazohusu umuhimu wa kuwapatia elimu watoto wote na kutowakatisha masomo na kuwaozesha.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo