• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MILIONI 30 KUNUFAISHA VIKUNDI 30 VYA WAJASIRIAMALI

Posted on: October 28th, 2019


Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Shukuru Kawambwa leo amekabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 30, 801,000 kwa Vikundi 30 vya vikundi vya wajasiriamali wanawake, Vijana na Wazee ili ziwasaidie katika shughuli zao za ujasiriamali.

Hafla ya kukabidhi Fedha hizo ambazo ni ruzuku toka mfuko wa Jimbo, imefanyika mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo wawakilishi wa vikundi vilivyonufaika vimekabidhiwa fedha hizo ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo kugawa fedha za mfuko wa jimbo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuchochea maendeleo katika shughuli za kiuchumi wanazofanya.

“Katika ugawaji wa fedha hizi kila kikundi kimeangaliwa vizuri, vikundi vya vijana, wazee na wanawake, hakukuwa na ubaguzi, lengo likiwa ni kuhakikisha tunawafikia walengwa na kuwasaidia kuzifikia ndoto zao kwa kuwawezesha kidogo ili twende mbele pamoja kiuchumi” Amesema Mhe. Kawambwa.

Ameongeza kuwa, baada ya ugawaji wa fedha hizo, atashirikiana na Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kuwatembelea wanavikundi waliopokea fedha hizo za ruzuku ili kuona kama fedha zilizotolewa zimekwenda kufanya kazi iliyokusudiwa, hivyo akatumia fursa hiyo kuwaasa wanavikundi wanufaika wa fedha hizo kuhakikisha wanakwenda kuzitumia vizuri fedha hizo ili kufikia malengo waliyojiwekea na kwa kufanya hivyo watakuwa wameionesha Serikali kuwa wanaweza kujiimarisha kiuchumi na kupiga hatua kimaendeleo pale wanapowezeshwa.

Mhe. Kawambwa pia ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wananchi wa Bagamoyo, kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali vya Wanawake, wenye ulemavu na Vijana katika maeneo yao, na kisha kuwasilisha maombi ya mikopo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kwani kuna fursa ya kuwezeshwa mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ujasiriamali wanazofanya.

“Katika Mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, imetenga jumla ya Shilingi Milioni 211,915,000/- toka mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa Vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu, robo ya fedha hizi hutolewa mara moja kila baada ya miezi 3, na ili mzipate ni lazima muwe mmejiunga katika vikundi vya wajasiriamali. Shime Wanawake, Wenye ulemavu na Vijana wa Bagamoyo, changamkieni fursa hii ya mikopo toka Halmashauri ili mkazitumie katika kuendeleza shughuli zenu za ujasiriamali, mjikwamue kiuchumi na wote kwa pamoja tuliletee Taifa letu maendeleo chanya” Amesema Mhe. Kawambwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Shukuru Kawambwa kwa kuiunga mkono Halmashauri katika kuwasaidia Wananchi kujikwamua kiuchumi, lakini pia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani baadhi ya fedha hizo za Mfuko wa Jimbo, pia zimetolewa kwa baadhi ya taasisi za Serikali zinazoendelea na miradi ya Ujenzi, zikiwemo Shule za Msingi, Sekondari na Zahanati.

“Kwa Miaka minne mfululizo Mfuko wa Jimbo la Bagamoyo, umekuwa ukitoa wastani wa Shilingi Milioni 30 kwa taasisi za Serikali na Vikundi vya wajasiriamali wadogo ndani ya Halmashauri, ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwetu kama Halmashauri, lakini pia kwa wajasiriamali ambao wamekuwa wakinufaika na fedha hizo wanazopokea ili kuchochea maendeleo ya shughuli zao za Ujasiriamali wanazofanya katika kujikwamua kiuchumi” Amesema Bi. Fatuma.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Alli Alli Issa, ametumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, mhe. Shukuru Kawambwa kwa kuwa na moyo wa kujitolea kwani ana hiyari ya kuelekeza fedha hizo katika shughuli zingine, lakini ameona ni vyema kuendelea kuwawezesha wajasiriamali wa Bagamoyo kiuchumi na kwa kufanya hivyo anashiriki kukuza uchumi wa Bagamoyo, na hilo ni jambo la kupigiwa mfano.

Mmoja wa Wanufaika wa ruzuku hiyo ya mfuko wa Jimbo, Mzee Golden Mwenda, toka kikundi cha Unjacha kilichopo Chasimba, Kata ya Yombo, ambao wanajihusisha na kilimo cha muhogo, amepongeza hatua hiyo ya utoaji fedha za ruzuku kwa vikundi vya Wajasiriamali wadogo.

“Nimefarijika sana, hii ni chachu kubwa kwetu, tunamshukuru Mhe. Mbunge wetu wa Jimbo la Bagamoyo, na Serikali kwa ujumla, kwani tunajionea jinsi inavyotujali wazee tusiojiweza, kutuwezesha kujikwamua kiuchumi na kujitegemea, hakika hatujasahaulika, ni faraja kubwa kwetu” Amesema Mzee Mwenda.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo