• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MIRADI TISA YA MAENDELEO YAKAGULIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO

Posted on: September 6th, 2017



Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Pwani, Ndugu Edward Bruno Mwakipesile jana ameongoza timu ya wataalamu ya Mkoa na Halmashauri kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri katika Kata ya Dunda, Mapinga, Kerege, Yombo, Makurunge na Fukayosi.

Miradi hiyo tisa yenye thamani ya Sh. 413,799,263/= ni ya sekta ya Afya, Maji, Elimu Msingi na Sekondari, Utawala na Maendeleo ya jamii na inatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kutokana na fedha za makusanyo ya ndani, Mfuko wa jimbo, Ruzuku ya kata na Vijiji, michango ya Wananchi na Wahisani mbalimbali.

Katika ukaguzi huo Wataalamu walioneshwa kuridhirishwa na ubora wa miradi na thamani halisi ya fedha zilizotumika kutekeleza miradi hiyo ambapo Ndg. Mwakipesile amesema “Natoa pongezi kwa Halmashauri, Wananchi na Wadau mbali mbali wa maendeleo kwa kutoa ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa miradi hii, kwani kwa kufanya hivyo huipunguzia serikali mzigo mkubwa na kuiletea jamii maendeleo ya haraka”.

Wakati huo huo kikundi cha kina mama cha Jitegemee Sacoss na kikundi cha Vijana waendesha bodaboda (UWADEPIMASHU) vyote vya Mapinga Wilayani Bagamoyo ambavyo vilitembelewa katika ukaguzi huo vilipongezwa kwa kujiunga pamoja na kufanya shughuli za kujiletea maendeleo na hivyo kuondoa utegemezi kwa kuweza kujiajiri na kupunguza changamoto za ajira Nchini.

Ndugu Mwakipesile pia akatumia fursa hiyo kuwaasa Wananchi ambao ndio wanufaika wakuu wa miradi hiyo ya maendeleo kuithamini na kuilinda ili iweze kuwanufaisha kwa muda mrefu huku akitoa ushauri kwa Wataalamu wa Halmashauri juu ya namna ya  kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokea wakati wa utekelezaji wa miradi  ikiwemo mwamko mdogo wa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo, uharibifu wa miundombinu hasa ya maji na rasilimali fedha.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo