• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA BILIONI 10 YATEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU BAGAMOYO

Posted on: July 19th, 2018


Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mapema leo asubuhi ya tarehe 19 Julai, 2018 ambapo ukiwa Wilayani hapa umeweka mawe ya msingi katika miradi miwil (2) na kutembelea miradi 10, yote ikiwa na thamani ya Shilingi Bilioni 10,863,514,920.04/=

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Hemed Mwanga ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Halmashauri ya Kibaha vijijini, yaliyofanyika katika Kijiji cha Miswe Wilayani Kibaha.

Mhe. Mwanga anasema kati ya fedha hizo, Shilingi Milioni 722,167,800/= ni miradi iliyotekelezwa na wajasiriamali wadogo, Milioni 14,116,620.7 ni miradi iliyotekelezwa kwa nguvu za Wananchi, Milioni 667,242,597.9 Wahisani, Bilioni 9,333,936,649.51 miradi iliyotekelezwa kwa fedha toka Serikali kuu, huku Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ikichangia kiasi cha Shilingi Milioni 126,051,251.97 katika miradi hiyo ya maendeleo.

Miradi hii toka sekta za Afya, Elimu, Utawala bora, maendeleo ya jamii, miundo mbinu ya barabara, maji na biashara imetekelezwa katika Kata za Kerege, Zinga, Magomeni, Dunda na Yombo ikiwa na lengo la kuboresha utoaji huduma bora kwa jamii hususani katika ya Elimu na Afya.

Aidha, Mhe. Mwanga amesema katika kutekeleza kwa vitendo Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2018 inayosema “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu”, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaendeleza Ujenzi wa vyumba 86 vya madarasa, ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi madarasani, lakini pia, inajenga Shule 8 mpya za Msingi na kuendeleza ujenzi wa maabara 16 katika Shule za Sekondari.

Nae Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2018, Ndugu Charles Francis Kabeho, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa utekelezaji wa mradi bora wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kerege, mradi ulioshika namba moja Nchini katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya Afya unaoendelea katika Halmashauri zote Nchini, kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, na kugharimu jumla ya Shilingi Milioni 500.

“Kituo hiki cha Afya Kerege ni Kituo bora, chenye majengo yaliyojengwa kwa viwango na kimekamilika na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi, nawapongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kusimamia vyema ujenzi wa mradi huu, lakini niiombe Bodi ya dawa Nchini -MSD kuharakisha kukamilisha uletaji wa vifaa tiba katika Kituo hiki cha Afya ili kiweze kuendelea na utoaji huduma kwa ukamilifu wake kama ilivyokususdiwa na Serikali”, Amesema Kabeho.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo umekimbizwa katika jumla ya Kilomita 169, na umekabidhiwa kwa Halmashauri ya Kibaha Vijijini ambako utakimbizwa Kilomita 69.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo