• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MKURUGENZI BAGAMOYO ASIKILIZA KERO ZA WAZEE

Posted on: June 12th, 2018


Wazee takribani 70 toka katika 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, wamepata fursa ya kukaa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri na kuelezea changamoto wanazokumbana nazo katika mkutano maalum uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.

Hatua hii imefikiwa na Viongozi hao wa Halmashauri ikiwa ni katika kuhakikisha Wazee ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wanatambulika na kushirikishwa katika maamuzi muhimu yanayowahusu wao na Halmashauri kwa ujumla.

Wazee hao kupitia mkutano huo pia walipata fursa ya kuelezea changamoto kadha wa kadha wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila siku na kupendekeza namna bora ya Serikali kuzitatua changamoto hizo.

Bibi. Rehema Juma (67) toka Kata ya Kerege akizungumza katika mkutano huo amesema, Wazee wamekuwa wakinyanyaswa na kudharaulika kila wanapokwenda katika Zahanati, Vituo vya afya na Hospitali kupata huduma za afya kwani bado kuna wahudumu wa Afya wenye lugha za kukatisha tamaa kwa Wazee, hivyo ofisi ya Mkurugenzi ifuatilie na kuona namna ya kuwashughulikia wahudumu wa Afya wanaonyanyasa Wazee wanapokwenda kupata huduma katika vituo hivyo.

Nae Mzee Alphonce Peter Mwandemo (64) toka Kata ya Magomeni, nae akaongeza kuwa ni vyema mchakato wa uundaji wa mabaraza ya Wazee ya Kata ukaharakishwa na kusimamiwa ipasavyo na Watendaji wa Kata ili kuhakikisha mabaraza hayo yanaundwa na yanaanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili Wazee wawe na sehemu sahihi ya kuzungumzia changamoto zao ili Halmashauri na Serikali kwa ujumla izifahamu na kutengeneza utaratibu maalum wa kuzitatua kwa haraka na kwa wakati.

Hali kadhalika, Mzee Charles Gideon (58) kutoka Kata ya Mapinga, yeye akashauri kuwa, Wazee ambao bado wana uwezo wa kujishughulisha na kujiingizia kipato wawezeshwe kupata mitaji ili wawekeze katika shughuli za kuwaingizia kipato kitakachowawezesha kuendesha maisha yao na kuweza kupata mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Pia Bibi. Ellen Majiba (72) toka Kata ya Zinga yeye akawashauri Wazee wenzake kuishi kwa upendo na kusaidiana hasa pale mmoja wao anapokuwa na shida kama kukosa chakula, mavazi ama malazi, wajaliane wao kwa wao, waoneane huruma na wasaidiane kwa wale wasiojiweza kwani umoja ni nguvu na utengano niudhaifu.

Akizungumza na Wazee hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Alli Alli Issa amesema, kikao hicho cha Wazee ni mwanzo tu, kwani yeye na Mkurugenzi wa Halmashauri wataendelea na utaratibu huo wa kukaa na Wazee, kuwatambua na kuwaunga mkono na kuwasikiliza kwani Wazee ni hazina isiyokauka na rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Fatuma Latu amewatia moyo Wazee hao kuwa Serikali ya Awamu ya tano ni Serikali Sikivu, ya wanyonge, yenye huruma kwa Wazee, Wakina mama, watoto na wasiojiweza hivyo Halmashauri itahakikisha inazishughulikia changamoto zote zilizotajwa ili Wazee ndani ya Halmashauri ya Bagamoyo waishi kwa Amani na kufurahia uzee wao.

Mkurugenzi anasema, “Tunaendelea kuboresha huduma katika hospitali ya wilaya, tumenunua mashuka zaidi ya 600 hapo kabla baadhi ya wagonjwa walikuwa wanalala bila shuka, lakini pia kupitia ofisi ya Ustawi wa jamii tutahakikisha tunapita katika mabaraza ya Wazee ya Kata yanayoendelea kuundwa katika Kata zote hivi sasa, ili kutoa elimu ya namna ya kuenenda katika mabaraza hayo. Msivunjike moyo, Hata wahudumu wa Afya katika Vituo vyetu vya Afya pia tutahakikisha tunawaboresha ili muanze kupata huduma mnazostahili bila kubughudhiwa”

Akaongeza, tutaendelea kujifunza kwa wenzetu kwa maana ya Halmashauri zingine zinazofanya vizuri katika utoaji huduma bora kwa wazee hasa katika sekta ya Afya ili na sisi tusibaki nyuma katika kuhudumia wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Anasema Mkurugenzi.

Bi. Latu akahitimisha kwa kuwanasibu Wazee hao wa Bagamoyo ambao bado wanamiliki ardhi, kutouza maeneo yao yote wakayamaliza, kwani watakosa maeneo ya kulima na kuzalisha malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyoendelea kujengwa ndani ya Halmashauri ya Bagamoyo, na hivyo kupelekea kukosa kunufaika na Tanzania ya viwanda ijayo.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo