• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MKURUGENZI MTENDAJI BAGAMOYO AFUNGA MAFUNZO YA WALIMU JAMII WASAIDIZI MRADI WA UTAYARI WA KUANZA SHULE..

Posted on: October 20th, 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Bwana Shauri Selenda  amefunga mafunzo maalumu ya walimu jamii wasaidizi jana Jumatano katiaka Shule ya Sekondari Bagamoyo Mkoani Pwani. Akifunga mafunzo hayo kama awali aliwapongeza  na kuwashukuru mradi wa Shule Bora kwa kuandaa  mafunzo hayo katika muda muafaka. Aliwashauri walimu waliopata mafunzo kutumia ujuzi walioupata katika mafunzo hayo  kukuza na  kuendeleza elimu katika vituo vya utayari wa kuanza  shule  watakavyopangiwa. Alisisitiza kuwa elimu ndio muhimu zaidi katika maisha kwani inampa mtu uwezo wa kukabiliana na maisha katika mazingira yoyote. ”Elimu ni muhimu sana katika kuleta maendeleo katika Nchi’’ alisisitiza Bwana Selenda. Kwa upande mwingine mgeni rasmi aliwashukuru wakufunzi kwa ubunifu mkubwa katika mafunzo hayo kwa kuwafundisha walimu jamii wasaidizi kupitia elimu  waliyopewa na kuwajengea maarifa. ” Nashukuru sana wakufunzi kwa kweli mmefanya kazi kubwa kuwajengea uwezo walimu hawa hasa kuwezesha kujifunza zana za ufundishaji kutokana na mazingira yao, huu ni ubunifu mkubwa  nawashukuru sana sana’’ alihitimisha Bwana Selenda.

        Akimkaribisha mgeni rasmi kabla ya kufunga mafunzo hayo, Afisa Elimu ya Awali na Msingi  Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Bi Wema Kajigili alimfahamisha mgeni rasmi  kuwa, chimbuko kubwa la kuanzisha mpango wa utayari wa kuanza shule ni changamoto iliyonekana huko nyuma kuwa, Kimkoa kuna shida kubwa ya watoto wakifika darasa la nne hawajui kusoma na kuandika ndipo ilibuniwa programu hii kuwasaidia watoto walioshindwa kupata mafunzo ya awali wapate mafunzo haya. ‘’ Tunategemea kendesha mafunzo haya watoto ya utayari wa kuanza shule kwa muda wa  wiki 12 na baada ya hapo watoto hao wataingia shule mama kuendelea na masomo ‘’ aliesma Bi Kajigiri. Mafunzo haya ya Utayari wa Kuanza Shule yaliendeshwa kwa miongozo na mitaala iliyotayarishwa na Tasisi ya Elimu na inajikita katika sehemu kuu Tano ikiwemo kuwawezesha walimu jamii wasidizi kuwafundisha watoto mawasiliano kwa lugha ya Kiswahili, utambuzi wa vitu mbalimbali kama picha,mahusiano, kujenga afya na utunzaji wa mazingira na usafi.  Kwa Mkoa wa Pwani vimeanzishwa vituo 36 vitakavyo toa elimu na kuna jumla ya walimu jamii wasaidizi 38 waliopatiwa mafunzo.

 

       Mpango wa Utayari wa Kuanza Shule ni mradi  chini ya Programu ya Shule Bora Nchini unaotelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Cambridge Education Tanzania.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo