• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MKURUGENZI MTENDAJI BAGAMOYO AKUTANA NA VIONGOZI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.

Posted on: August 17th, 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Ndg. Shauri Selenda  tarehe 17 Agosti  2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo amekutana na viongozi na wawakilishi wa  tassisi zisizo za Kiserikali (NGOs) ili kujadili  taarifa Mbalimbali za utendaji kazi wa tasisi hizo kwa Mwaka wa fedha 2021/2022.

      Akifungaua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji aliwasisitiza viongozi hao kufanya kazi kwa kufuata misingi ya katiba na taratibu za Nchi kuhakikisha kuwa wanawasaidia wananchi pamoja na kuleta maendeleo. ‘’Najua lengo la taasisi zenu ni kuwasaidia na kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo Mbalimbali hivyo nawasihi kuwa lazima mfanye kazi kwa taratibu na sheria zilizopo, sisi kama Serikali tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na Tasisi hizi zisizo za Kiserikali ila hatutasita kuuingilia kati pale tutakapoona tasisi zenu zinaenda kinyume na matakwa ya sheria’’ alisema Mkurugenzi huyo. Ailwafahamisha viongozi hao kuwa wakati wote Serikali ipo tayari kufanya kazi na tasisi zote kunafanikisha malengo ya kuwapa huduma na maendeleo wananchi hasa wa kipato cha chini.

      Wakiwasilisha taarifa Mbalimbali za utendaji kazi wa taasisi hizo kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 na mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kusomesha watoto 489 katika shule za awali,msingi,sekeondari na vyuo amabapo moja kati yao wavulana ni 207 na wasichana ni 282. Walieleza kuwa, utoaji wa elimu kwa wanufaika ulijikita hasa katika masuala ya elimu ya jamii,hasa haki za watoto,ukatili wa kijinsia, masuala ya mirathi,wosia na masuala ya ujasiriamali. Aidha viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali walimtaarifu Mkurugenzi Mtendaji kuwa,watu wapatao 3,408 walipata mafunzo kuhusu masuala ya ardhi kwani kwa maoni yao Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ni moja kati ya halmashauri inayoongoza kwa migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Pwani. ‘’Mhe.mageni rasmi pamoja na mafanikio yote hasa kuhusu kazi zetu za kawaida tumefanikiwa pia kuwapa elimu vijana 437 kuhamasisha na kutoa elimu ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022 haya nai mafanikioa makubwa kwa uapande wetu ‘’ alisema Mwakilisha wa taasisi ya Rafiki Tanzania (RATA). Katika kikaokazi hicho jumla ya taasisi zaidi ya 6 sizizo za Kiserikali zilihudhuria katika kikao hicho ikiwemo Taasisi ya Rafiki Tanzania(RATA), Moyo Mmoja , Dynamic Women For Productive Initiative,(DWOPRI), Amazing Step For Children Foundation na Bagamoyo BACCA. Kauli mbiu ya Mashirika hayo yasiyo ya Kiserikali katika utekelzaji wa kazi zao ilikuwa ‘’ Uendelevu wa Mashirika asiyokuwa ya Kiserikali; Wadau Tuwajibike’’

   Kwa upande wake, mratibu wa masuala ya taasisi zisizo za Kiserikali Halmashauri wa Wilaya Bagamoyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi Delvin Maleko aliwashukuru viongozi hao wa taasisi hizo kwa kupata muda wa kujadili taarifa zao za Mwaka na kuhaidi kuwa, Idara yake imepokea changamoto zote zilizoelezwa katika kikao na zitafanyiwa kazi ili kuleta tija na maendeleo yaliyokusudiwa na taasisi hizo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo