• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MOTO WATEKETEZA MELI BAGAMOYO

Posted on: August 14th, 2018



Meli kubwa ya mizigo iitwayo MV RAHIMA (LAND CRAFT RAHIMA) imeungua moto kwa asilimia 20% mapema leo asubuhi ya Tarehe 14/08/2018 katika bandari ya Bagamoyo.
Meli hiyo inayomilikiwa na Ndg. Hamis Rashid mkazi wa Unguja ilikua ikiongozwa na Kapteni Abdulrahman Abdulaziz ambaye pia ni Mkazi wa Unguja na ina uwezo wa kubeba mzigo wenye ukubwa wa Tani 500 kwa mara moja.
MV RAHIMA imekaa kwa muda wa wiki moja katika Bandari ya Bagamoyo ikisubiri kupakia mzigo wa Saruji wa Tani 300 na ndani ya Meli kulikua na jumla ya watu 16 ambao ni mabaharia na wafanyakazi wengine wa Meli.
Kwa mujibu wa Kapteni wa Meli hiyo Bw. Abdulrahman Abdulaziz ni hitilafu ya umeme na anaongeza kusema, “Mlango wa mbele wa Meli ulikua umeharibika, hivyo Alfajiri ya Tarehe 14 Agosti, 2018, tuliamkia kuutengeneza kwa kuuchomelea tayari kwa kujiandaa kupokea mzigo na kuanza safari ya kurudi Unguja” Anasema Bw. Abdulrahman.
Anaongeza, Wakati tunatengeneza mlango huo, ghafla tuliona moshi mkubwa eneo analokaa kapteni wa Meli kuongoza Meli, na hivyo kutulazimu kusitisha zoezi la kuchomelea mlango na kwenda kuangalia sababu ya Moshi huo, ambapo tulikuta eneo la chumba cha kapteni likungua moto uliosababishwa na hitilafu ya Umeme.
Bw. Abdulrahman anabainisha kuwa, Moto huo ulianzia katika chumba cha kepteni wa Meli mnamo saa 11:45 Asubuhi na taarifa zilifika kituoni katika Jeshi la Zimamoto saa 12:25, Zimamoto walifika eneo la tukio saa   12:30 na walifanikiwa kuzima kabisa moto mnamo saa 1:30 Asubuhi.
Anaongeza, eneo ambalo moto umetokea lina vyumba sita vya abiria ambavyo vyote vimeungua, na wakati moto unaanza kulikua na mabaharia wawili vyumbani wamelala lakini wote wametoka salama.
Vitu ambavyo wamepoteza kutokana na moto huo ni pamoja na nguo, Fedha, Vitanda pia Vifaa vya kuongozea meli vyote vimeungua hata hivyo hakuna taarifa ya Kifo wala majeruhi aliyeripotiwa katika ajali ya hiyo.
Meli ya MV RAHIMA imesajiliwa huko visiwani Zanzibar na ina vibali vyote vya usajili ambavyo vyote vimeungua moto katika ajali hiyo, hata hivyo, hajui Meli hiyo ilisajiliwa Mwaka gani ila imefanyiwa ukaguzi Mwaka huu huko Pemba lakini anakiri kuwa hajui ni lini hasa imefanyiwa ukaguzi huo kwa maana ya Tarehe na Mwezi na pia Mamlaka iliyokagua meli hiyo pia haifahamu.
Nae Kamanda wa Zimamoto Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Hiward Mwanza baada ya ukaguzi wa Meli hiyo anabainisha yafuatayo kuwa, Meli hiyo ina vizimia moto vitatu vikuu kuu ambavyo vinaonesha vinatakiwa kufanyiwa tena ukarabati Januari 2019
Anaongeza, Meli ina mfumo wa kuzimia moto lakini Kapteni anasema mfumo huo haufanyi kazi, Meli haina Mlango wa dharura wa kutokea nje inapotokea ajali au hatari, pia haina alama za zinazoonesha dharura mfano Emergency Exit, Mfumo wa utoaji maji kwenye Meli umeoza na mabaharia hawana mafunzo ya kujikinga na moto pia Meli haina vifaa vya zimamoto
Meli ya MV RAHIMA, Meli hii huja Bagamoyo mara mbili kwa Mwezi kuchukua Saruji, na kila mara inapokuja Bandari ya Bagamoyo hubeba Tani 300 – 500 za Saruji.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo