• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

RC NDIKILO APONGEZA MPANGO WA TASAF WA AJIRA ZA MUDA KWA WALENGWA

Posted on: June 26th, 2018



Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo amepongeza mpango wa ajira za muda kwa walengwa wa TASAF Wilayani Bagamoyo, unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF.
Mhe. Ndikilo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara maalum ya kutembelea na kukagua miradi ya ajira za muda zinazotekelezwa na walengwa wa TASAF Wilayani Bagamoyo ambapo alitembelea mradi wa upandaji wa Miti ya Mikoko pembezoni mwa Pwani ya bahari ya hindi katika Kijiji cha Kondo kilichopo Kata ya Zinga na mradi wa Ujenzi wa Lambo uliopo katika Kijiji cha Rupungwi Kata ya Mandera.
Walengwa hao wa TASAF huibua miradi mbalimbali katika maeneo yao na kuitekeleza chini ya mpango TASAF wa ajira za muda kisha kulipwa ujira kupitia utekelezaji wa miradi hiyo ambayo kwa Wilaya ya Bagamoyo walengwa wamekua wakitekeleza miradi ya upandaji miti, ukarabati wa barabara za jamii, ujenzi na ukarabati wa malambo, ukarabati wa viwanja vya michezo, uchimbaji wa visima, uhifadhi vyanzo vya maji, ukarabati na ujenzi wa mabwawa na visima.
“TASAF imekua mkombozi kwa Wananchi masikini katika Mkoa wa Pwani kwa kuwawezesha kupata milo mitatu kwa siku, kuanzisha miradi midogo midogo ya biashara na hivyo kujijengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi, kuboresha mahudhurio ya wanafunzi mashuleni na kwa watoto walio chini ya miaka mitano wanaotimiza masharti ya afya nao pia mahudhurio yao kliniki yameboreka anasema na Wananchi wameweza kukata bima ya afya kupitia mfuko wa Afya ya jamii CHF, bima inayowasaidia kujipatia uhakika wa matibabu wao na familia zao” Mhe. Eng. Ndikilo.
“Ni rai yangu kwa walengwa wanaoendelea kupokea ruzuku hii ya fedha toka mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kujiwekea malengo maalum ya kimaendeleo na kuyatimiza ikiwemo kuboresha makazi yenu kwa kujenga nyumba bora, niwakumbushe kuweka akiba lakini pia kuwekeza katika kufungua miradi endelevu ili mpango utakapofikia tamati msirudi katika umasikini mliokuwa nao awali bali msonge mbele mkiwa tayari na uwezo wa kujitegemea kiuchumi Anaongeza” Mhe. Eng. Ndikilo.
Akiwa katika Kijiji cha Rupungwi, Mkuu wa Mkoa Mhe. Eng. Evarist Ndikilo, pia alipata nafasi ya kushiriki zoezi la ugawaji fedha za ruzuku kwa Walengwa 75 wanaopatikana katika Kijiji hicho na kutumia fursa hiyo kuongea na Wananchi wa Kata ya Mandera akiwahimiza juu ya kuacha vitendo vya uhalifu kila mmoja kuwa mlinzi wa Mwenzake, kushiriki katika shughuli za ulinzi shirikishi ili kuhakikisha eneo hilo halitajwi katika vitendo vya kihalifu vya kuvamia magari na kupora maduka kwa magobore kama ilivyo sasa.
Programu ya ajira ya muda kwa walengwa wa mpango wa TASAF Wilayani Bagamoyo ilianza utekelezaji wake Mwaka 2015 ambapo katika mwaka wa fedha 2015/2016 jumla ya Tshs.1,292,761,000.00 zililipwa kwa Kaya za walengwa 10,363, Wanawake wakiwa 8,614 na Wanaume 1,749 huku miradi 14 ikiibuliwa na kutekelezwa na Walengwa na kwa Mwaka 2016/2017 miradi 98 iliibuliwa, ambapo Kaya 9,265 zilishiriki kufanya kazi za ajira kwa muda na kulipwa kiasi cha 1,215,064,700.00 na kwa Mwaka 2017/2018 jumla ya miradi 103 iliibuliwa na kutekelezwa ambapo jumla ya Kaya 8,330 zimeshiriki kufanay kazi za ajira kwa muda na kulipwa Tshs. 723,856,000.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo