• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

RC NDIKILO APONGEZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KEREGE BAGAMOYO

Posted on: March 22nd, 2018


Mkuu wa Mkoa wa pwani Mhe. Evarist Ndikilo ametoa pongezi hizo akiwa katika kituo kipya cha Afya Kerege, mapema leo asubuhi ya Tarehe 22.03.2018, alipokuwa kwenye ziara maalum ya kuvitembelea na kuvikagua  vituo vya Afya vilivyojengwa ndani ya Mkoa wa Pwani, chini ya utaratibu wa Serikali wa kutoa jumla ya Tshs. Mil 500 kwa kila Halmashauri nchini ili kuboresha miundo mbinu ya Afya.

Katika ziara hiyo Mhe. Ndikilo amepata fursa ya kujionea dhahiri namna ambavyo uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo umeitendea haki “force account” kwa kujenga kituo bora zaidi cha Afya nchini kitakachoanza kutoa huduma mapema hivi karibuni.

“ Niwapongeze sana, hakika mmejenga kituo cha Afya cha kupigiwa mfano Nchini, mmetumia fedha vizuri na hata mmevuka lengo la Serikali iliyopanga mjenge majengo manne (4) lakini Bagamoyo mmefanikiwa kujenga majengo 11 na yote yakiwa katika kiwango na ubora wa hali ya juu” Amesema Ndikilo.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Ndikilo akatumia fursa hiyo pia kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Majid Mwanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu, Waheshimiwa Madiwani, Kamati ya wataalamu wa Halmashauri, kamati mbalimbali za ujenzi na Wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kipindi chote cha ujenzi na kuwezesha kukamilisha ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Kerege kitakachowahudumia Wananchi wa Kata ya Kerege na Kata jirani.

Pia Mhe. Ndikilo akatoa ushauri kwa Uongozi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bagamoyo kutumia fedha za mapato ya ndani kuanza ununuzi wa vifaa tiba vingine vitakavyohitajika katika kituo hiko cha Afya, ambavyo havipo kwenye listi ya vifaa tiba vitakavyonunuliwa na Serikali kuu kwa ajili ya kituo hiko cha Afya vitakavyogharimu, Tsh. Mil 220, fedha itakayotolewa na Serikali kuu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika kituo hicho cha Afya sawa na mwongozo na maelekezo ya Serikali.

Wakati huo huo, Mhe Ndikilo ametoa Rai kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na Bima ya Afya, kwani Ugonjwa hautabiriki utakuja lini ingawa lengo la Serikali ni kuboresha huduma ya Afya na upatikanaji wa Dawa kwa vituo vyake vyote.

Akihitimisha Ziara yake hiyo kituoni hapo, Mkuu wa Mkoa amewaasa watumishi wa Sekta ya Afya kuwa na lugha nzuri na kutoa huduma bora kwa wananchi, na si bora huduma, kwani Uboreshaji wa huduma za Afya unaofanywa na Serikali hivi sasa Nchini, hailengi kuboresha miundombinu na kuwa na majengo bora pekee, bali pia inalenga utoaji bora wa huduma za Afya wenye kukidhi matakwa ya Wananchi na hasa wa hali ya chini na makundi maalum kama wazee, watoto na wakina mama wajawazito.

Ujenzi wa kituo cha afya kerege ulianza tarehe 20/10/2017 na ulitarajiwa kukamilika tarehe 15/01/2018 huku lengo kuu la mradi likiwa ni kuboresha vituo vya afya nchini na kuwa na vituo vya afya vyenye ufanisi.

Hadi mradi huu utakapokamilika, Kituo cha Afya Kerege kitakuwa na Jengo la upasuaji, Jengo la wazazi, Nyumba ya mtumishi, Jengo la maabara, Jengo kwa ajili ya mfumo wa umeme na jenereta, Mashimo mawili ya kuvunia maji, Minara miwili ya kuvunia maji yenye vyoo na stoo chini, Kichomea taka, Jengo la kufulia nguo na Jengo la kuhifadhia maiti.

Mradi umekadiriwa kugharimu jumla ya Tsh 544, 000,000.00 ambapo kiasi cha Tshs 500, 000,000.00 ilipokelewa kutoka OR-TAMISEMI na kiasi cha Tshs. 44,000,000 ni mchango wa Halmashauri.

Hadi sasa kiasi cha Tsh 478, 000,000.00 zimetumika ambapo kiasi cha Tshs 460, 000,000.00 kimetumika katika ujenzi na Tshs 18, 000,000 kimetumika katika shughuli za usimamizi wa mradi.

Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha kutolewa kwa huduma za Afya kwa ufanisi zaidi zikiwemo huduma za dharura na kufanya upasuaji kwa akina Mama (CeMOC).

Kituo cha Afya Kerege kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa Jumla ya  wananchi  7,114.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo