• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

SAMIA AAHIDI KERO ZA WANANCHI WA PANDE KUSHUGHULIKIWA

Posted on: October 24th, 2018


Wakazi wa Kitongoji cha Pande, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambao wamehamishwa kupisha mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo wameiomba serikali kuwasaidia kulipwa fidia na kuhamishiwa katika makazi mapya ya Kidagoni na Kitopeni kama walivyoaihidiwa na Serikali wakati wanakubaliana kupisha maeneo hayo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Akitoa kilio hicho kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo, wakati wa Ziara maalumu ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, alipotembelea na kukagua  eneo la mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo katika eneo la Mbegani mapema leo, Mwenyekiti wa kitongoji cha Pande Muhsin Mneka alisema  walipangiwa kwenda eneo la Kitopeni na Kidagoni lakini wameshindwa kwenda kutokana fidia kutokamilika na baadhi yao kutolipwa kabisa.

“Wapo wenzetu hapa waliolipwa hapa hadi laki moja, milioni tano na milioni moja kiasi ambacho hakikidhi Mwananchi kuondoka na kuhamia katika makazi mapya, japo hatujakataa kupisha mradi ila makubaliano yetu hayajatekelezwa, kwani EPZA na sisi tulikubaliana kwa maandishi kuwa tutaondoka katika maeneo yetu haya na wao kiutapatia maeneo mbadala ya Kidagoni na Kitopeni" Alisema Mneka.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa Kijiji hicho kina Jumla ya Kaya 2,200 sawa na watu 16,500 ambao wanatakiwa kuhama katika eneo hilo kupisha ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo lakini Wananchi hao.wamekumbwa na changamoto kubwa ya kupunjwa ama kutolipwa kabisa fidia zao hivyo kuna haja ya kuhakikisha suala hilo linafikia mwisho.

"Naiomba Serikali kupitia Mhe. Makamu wa Rais kututazama kwa jicho la huruma kuhakikisha Wananchi hawa wa Kitongoji cha Pande wanapata haki zao, lakini pia tunaiomba sana Serikali tukufu ya Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kuharakisha utekelezaji wa mradi huu kwani muda umekwenda sana tangu jiwe la Msingi la ujenzi wa Bandari hii lilipowekwa Mwezi Oktoba, 2015 na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete, tunaiomba sana Serikali ianze utekelezaji wa mradi huu wa bandari ya Bagamoyo ambayo itakuwa ndio bandari kubwa zaidi kuliko zote katika Pwani ya Afrika Mashariki, na tunaamini bandari hii itasaidia kukuza uchumi wa wana Bagamoyo na Taifa la Tanzania kwa ujumla". Alisema Mhe. Kawambwa

Akijibu hoja hizo, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Samia Suluhu Hassan alisema , suala hilo amelichukua na atalipeleka kwa Rais baada ya kukaa na mamlaka husika ,wizara ya ardhi, bandari na EPZA ili kulipatia ufumbuzi. na kuongeza kwamba malalamiko yote yatafanyiwa kazi na Serikali kamwe haitamdhulumu Mwananchi yeyote haki yake.

Akaongeza, "Nimesikia kuna watu takribani 600 ambao wakati wa malipo ya fidia ya watu wa Pande, walifika na kufanya udanganyifu na kuiibia Serikali kwa kupokea fidia za watu wa Pande ili hali wao si wakazi wa Kitongoji hiki na watu hawa mnawafahamu, lakini mliwaficha, mlikaa kimya na watu hao wakafanikiwa kuiibia Serikali fedha hizo, mlikosea sana kukaa kimya na kutowaripoti katika vyombo vya Ulinzi na Usalama ili washughulikiwe, na yamkini fedha hizo walizolipwa ndio ambazo mngelipwa ninyi wakazi halali wa Pande mnaolia hadi leo kwa kukosa fidia zenu, nichukue fursa hii kukemea kwa nguvu zote tabia hii ya kuficha uovu, lakini kuagiza vyombo vya Ulinzi na usalama kuhakikisha watu hao walioiibia Serikali wanatafutwa kokote walipo na kuhakikisha wanarudisha fedha hizo na kuchukuliwa hatua za kisheria" Alisema Mhe. Samia.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Samia Suluhu Hassan, yupo katika Ziara maalum ya kikazi ya siku tano Mkoani Pwani, akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo Mkoani humo, Ziara iliyoanzia Wilayani Bagamoyo siku ya Tarehe 24 Oktoba, 2018

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo