• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

SI KILA HOMA NI MALARIA

Posted on: April 26th, 2019


Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi, Mtendaji Mkuu wa Mji mdogo wa Bagamoyo, Ndg. Athumani Stili, alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa, katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika tarehe 25 Aprili, 2019

Maadhimisho hayo ambayo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo yamefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo iliyopo katika Kata ya Magomeni, yamefanyika kwa ushirikiano baina ya Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na Taasisi ya uchunguzi ya Ifakara Health Institute (ihi) ambapo wataalamu wa Afya toka vituo hivyo viwili walishirikiana kutoa huduma za upimaji wa ugonjwa wa malaria na matibabu kwa wananchi waliokutwa na ugonjwa huo, upimaji wa shinikizo la damu, upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI na huduma ya ushauri nasaha.


Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Ndg. Stili amesema, Wananchi wengi wamejijengea utamaduni wa kutumia dawa za malaria kila wanapopatwa na homa, kitu ambacho si sahihi kwani Si kila Homa ni Malaria.


“Nawasihi Wananchi wa Bagamoyo kuhakikisha kabla ya kutumia dawa za Malaria, wawe wamefika katika Vituo vya kutolea huduma za Afya, waonane na Wataalamu wa Afya na kupima, ili wapatiwe matibabu sahihi pale wanapopatwa na ugonjwa wa homa, kwani Si kila Homa ni Malaria, na matumizi mabaya ya dawa za malaria yanaweza kutengeneza usugu hivyo kupelekea mwili kushindwa kupokea matibabu ya malaria badae mwili unapohitaji matibabu hayo” Amesema Ndg. Stili.


Akaongeza, Ni vyema unaposikia dalili za malaria kuwahi mara moja katika Kituo cha kutolea huduma za Afya, ili upate matibabu stahili badala ya kukimbilia tu kununua dawa na kutumia au kutumia dawa za asili ambazo hazijathibitishwa kisayansi na Wataalamu wa Afya, kwani kwa kufanya hivi unaweza kupoteza maisha maana Malaria inaua.


Takwimu za ugonjwa wa Malaria Wilayani Bagamoyo, kwa mujibu wa mratibu wa ugonjwa wa malaria Wilayani Bagamoyo, Dkt. Zena Mtajuka zinaonesha kuwa kwa mwaka 2018 kati ya wagonjwa wote waliopatiwa matibabu kupitia kitengo cha wagonjwa wa nje yaani (OPD), 5% ya wagonjwa hao walikutwa na ugonjwa wa Malaria na walipatiwa matibabu ya ugonjwa huo.


Dkt. Zena pia amesema kupitia taarifa yake aliyoisoma mbele ya Mgeni rasmi kuwa, Halmashauri imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa matibabu sahihi ya ugonjwa wa malaria katika vituo vyote 27 vya kutolea huduma za Afya vilivyopo ndani ya Halmashauri, pia utoaji wa Vyandarua vyenye dawa ya kuzuia mbu waenezao malaria kwa wajawazito na watoto walio chini ya mwaka mmoja mara tu wanapoanza mahudhurio ya kliniki ya mama na mtoto.


Siku ya malaria Duniani huadhimishwa tarehe 25 Aprili kila Mwaka na kwa Mwaka huu maadhimisho haya yalibebwa na kauli mbiu isemayo “Zero Malaria inaanza na Mimi”

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo