• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI..

Posted on: May 29th, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia mipaka na majukumu yao katika utendaji wa kazi ili kuepusha migogoro na miingiliano katika kuwahudumia wananchi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Amesema ni lazima watendaji na viongozi wote wa kisiasa kufanya kazi kwa pamoja na kufanya mazungumzo ya kujenga kwa manufaa ya wananchi panapotokea hoja au mitazamo tofauti katika utekelezaji.

Aidha Makamu wa Rais amewasihi viongozi hao kutambua lengo kuu katika nyadhifa zao ni kuwaletea wananchi maendeleo na siyo migogoro baina yao hivyo ni muhimu kuheshimiana, kuwajibika, kushirikiana kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuondoa vikwazo vyovyote vinavyoweza kukwamisha miradi hiyo. Pia amehimiza ushirikiano baina ya Madiwani na Wakurugenzi wa Halmashauri na kuondokana na tabia ya Madiwani kutoa maazimio dhidi ya Wakurugenzi pamoja Wakurugenzi kutowaheshimu Madiwani.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewataka viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa Mapato na kudhibiti uvujaji wa mapato katika maeneo yao. Ametaja tathmini ya taarifa za mapato kutoka katika mfumo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na vyanzo vingine vilivyokusanywa kupitia mashine za POS imebaini katika baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa fedha hazipelekwi katika akaunti husika za benki hivyo amewasihi kuzingatia taratibu za fedha na kudhibiti matumizi yasiyo na tija.

Aidha amewahimiza Madiwani kusimamia vema Halmashauri zao na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato. Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa TAMISEMI kuwachukulia hatua mara moja Viongozi na Watumishi wanaobainika kufanya matumizi mabaya ya fedha za umma, vitendo ambavyo husababisha baadhi ya miradi ya maendeleo kutekelezwa kwa kiwango cha chini kwa kuwa fedha zilizopangwa kwenda kwenye mradi husika huenda kwenye mifuko ya viongozi na watumishi wasio waaminifu.

Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia utawala bora, kukomesha unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, usimamizi wa Nidhamu, Maadili na Uwajibikaji pamoja na kushirikiana na jamii katika kutoa elimu na kulinda maadili ya vijana. Pia ameagiza kuimarisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira pamoja na usafi ili kuwa na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki amewahimiza viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia vema Halmashauri pamoja na kuwahamasisha na kuwasimamia wananchi katika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo.

Pia amesema Wizara itaendelea kushirikiana vema na ALAT katika kuzisaidia Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuweka msukumo kwa Halmashauri 56 ambazo hazijafikia makusanyo ya shilingi bilioni 2 au zaidi kwa mwaka ili ziweze kuongeza mapato. Halikadhalika ameziasa Halmashauri kuwa chachu na tija katika kupokea wawekezaji na wafanyabiashara katika maeneo yao ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya uwekezaji na biashara bila vikwazo.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Constantine Sima amesema Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa imefanikiwa kuziunganisha na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwezesha kupungua kwa hati chafu za ukaguzi.

Ameongeza kwamba Jumuiya hiyo inasisitiza Halmashauri zote kuweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha thamani halisi ya fedha inaonekana katika miradi inayotekelezwa. Amesema mkutano huo ni jukwaa la kubadilisha uzoefu, maarifa na mifano bora katika uendeshaji wa Serikali za Mitaa.

Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Miundombinu iliyoboreshwa ni chachu ya utoaji wa huduma bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa"

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo