• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TANZANIA BILA MAGONJWA YA MLIPUKO INAWEZEKANA

Posted on: July 29th, 2020

Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za Afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni pia kutumia vitakasa mikono.

Timu kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa umma cha Wizara ya Afya wakishirikiana na wataalam wa Mkoa na Shirika la Red Cross Tanzania wapo katika kampeni maalum ya kuelimisha umma juu ya masuala ya Afya, hususani wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii yaani CHF iliyoboreshwa, kuzingatia lishe bora, umuhimu wa kuhudhuria kliniki ya mama na mtoto katika vituo vya kutolea huduma za Afya na uchukuaji tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko kama kuhara na kipindu pindu.

Afisa muelimishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ndg. David Muya, akizungumza na walimu na wanafunzi takribani 2378 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Wilayani hapa, katika Shule ya Msingi Majengo na Jitegemee zilizopo katika Kata ya Magomeni, amesema, ni muhimu wazazi, walimu, wanafunzi na jamii nzima inashiriki kikamilifu kutokomeza magonjwa ya mlipuko kama ilivyofanya kwa mlipuko wa ugonjwa wa corona uliotokea hapa Nchini, miezi minne iliyopita kwa kuendelea kuchukua tahadhari zile zile za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, pia kutumia vitakasa mikono.

“Ninyi ni wajumbe wazuri, tumefika hapa leo ili mtusaidie kufikisha ujumbe huu kwa wazazi na walezi mtakaporudi majumbani, tumeishinda corona kwa kuzingatia maelekezo tuliyokuwa tukipewa na wataalam wa Afya, endeleeni kuzingatia maelekezo yale ili kujiepusha magonjwa mengine ya mlipuko ili Tanzania ibaki kuwa salama kwani Tanzania bila magonjwa ya mlipuko inawezekana” Amesema Bw. Muya

Anaongeza, “ili jamii yetu iwe salama, ni muhimu kuzingatia lishe bora wakati wote, wakumbusheni wazazi na walezi kuzingatia upatikanaji wa mlo kamili katika kaya zenu, pia kujiunga katika mfuko wa bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa yaani CHF iliyoboreshwa ili kupata uhakika wa matibabu pale mmoja wa wanafamilia atakapohitaji huduma za Kiafya, bima hii inapatikana katika Ofisi za Vitongoji mnavyoishi kwa gharama ya Shilingi 30,000/- tu, ambapo wanafamilia 06 watanufaika na huduma hii ya bima ya Afya kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali ya Wilaya na hata Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani”

Kampeni hii inaendeshwa kwa muda wa siku tatu ambapo imeanza leo tarehe 29 Julai 2020 na itakamilika tarehe 31 Julai, 2020 ikitarajiwa kuzifikia Kata zote 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, ambapo siku ya leo kampeni imefanyika katika Kata za Magomeni, Kisutu, Nia njema na Dunda elimu ya Afya Kinga imetolewa katika makundi ya watu mbali mbali katika maeneo hayo, hususani maeneo yenye mikusanyiko ya watu, Shuleni, Vyuoni, viwandani na kwenye masoko.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo