• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TATHIMINI YA WEPMO KUELEKEA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI TAREHE 15 OKTOBA, 2018

Posted on: October 8th, 2018

Kuelekea kuadhimisha kilele cha siku ya Unawaji mikono Duniani, ambayo hufanyika kila Mwaka ifikapo tarehe 15 Oktoba, Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wamehimizwa kujenga tabia ya kunawa mikono kila mara na kuwa na vifaa vya unawaji mikono kando ya vyoo vyao ili kujiepusha na magonjwa yanayotokana na uchafu wa kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni.

Wito huo umetolewa na Meneja mradi wa Shirika la Water and Environmental Sanitation Project Maintanance Organization (WEPMO) Tanzania, Bw. Renatus Rweyemamu, linalotekeleza mradi wa uboreshaji Afya na Usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, alipokuwa akitoa tathmini ya utekelezaji wa mradi huo kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya unawaji mikono Duniani.

Meneja mradi huyo anatanabaisha kuwa tarehe 18 -20 Septemba, 2018 wamefanya ufuatiliaji katika Kata ya Makurunge Wilayani Bagamoyo kuona muitikio wa uhamasishaji walioufanya juu ya ujenzi wa vyoo bora na uwekaji wa vinawia mikono katika kila Kaya ambapo Wananchi wameonesha muitikio chanya wa kujenga vyoo bora vya kudumu na kuweka vinawia mikono katika Kaya zao.


Nae Afisa Afya toka Kata ya Makurunge katika Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo Ndg. Ludamila Mgalula, amesema utekelezaji wa mradi wa uboreshaji  afya na usafi wa Mazingira chini ya Shirika la WEPMO- Tanzania, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo umekuwa ni msaada mkubwa kwani wamesaidia kuhamasisha jamii  juu ya ujenzi wa vyoo bora na uwekaji wa vinawia mikono lakini pia kuhakikisha kuwa unawaji mikono baada ya kutoka chooni unazingatiwa.


Anaongeza “Nashukuru sana Shirika la WEPMO- Tanzania kwa kusaidia zoezi la uhamasishaji na ufuatilaji wa kuhakikisha kuwa kila Kaya inakuwa na choo bora chenye kifaa cha kunawia mikono katika Kata ya Makurunge na nawaahidi kwamba, Kata itahakikisha inaendeleza juhudi za uhamasishaji na ufuatiliaji kupitia sheria ndogondogo za kata na mabaraza ya kata kutoa adhabu kwa watu wote watakaokiuka kanuni bora za afya”. Anasema Bw. Mgalula


Utafiti wa awali uliofanywa na shirika WEPMO katika Kata 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo unaonesha kuwa ni 23% tu ya Kaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wana vifaa vya kunawia mikono nje ya vyoo vyao.  

Aidha Afisa mradi toka Shirika la WEPMO Bw. Denis Mkani amesema wamefanya uhamasishaji kwa muda wa miezi minne katika Kata 11 za Halmashauri juu ya ujenzi wa vyoo bora vinavyoambatana na vinawia mikono katika kila Kata na Wananchi wameonesha kubadilika kwa kiasi kikubwa.


Bw. Mkani pia ametoa wito kwa Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kujenga tabia ya kunawa mikono mara watokapo chooni, kabla ya kula pia baada ya kutoka kwenye shughuli mbalimbali na kusisitiza matumizi bora ya vyoo kwa kuzingatia usafi ili kujiepusha na magonjwa yanayotokana na kutozingatia kanuni bora za afya, kwani suala la afya na usafi wa mazingira ni jukumu la kila mtu na kwa kushirikiana Halmashauri, uhamasishaji utaendelea kufanyika ili kuhakikisha kiwango kinaongezeka cha kaya zenye vifaa vya kunawa mikono na zinazingatia unawaji mikono na kanuni nyingine za afya.


Mradi wa uboreshaji Afya na usafi wa mazingira unatekelezwa na Shirika la WEPMO, linalofadhiliwa na USAID na ni shirika linalofanya kazi ya kuisadia Serikali katika kutekeleza kampeni ya Taifa ya uhamasishaji ujenzi wa vyoo bora maarufu kama ‘USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO’ mradi unaotelezwa kwa Mwaka mmoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na utarajiwa kukamilika Mwezi Mei, 2019


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo