• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TUZINGATIE LISHE BORA NA MAZOEZI KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: October 14th, 2020

Hayo yamesemwa leo Oktoba 14,2020 na Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni, katika maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo kwa Wananchi kupatatiwa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza, vipimo na matibabu bure.

Akizungumza katika kumbukizi hiyo Bi. Kasilda amesema ni Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius K. Nyerere enzi za uhai wake alisisitiza Wananchi kupiga vita Ujinga, Umaskini na Maradhi na katika kumuenzi na kuishi falsafa yake hiyo Halmashauri imeamua kumkumbuka katika siku hii muhimu ya kumbukizi ya kifo chake kwa Wataalam wa Afya kutoa elimu ya Afya kinga na Afya Tiba juu ya magonjwa yasiyoambukiza ili jamii ipate uelewa wa namna ya kuepukana na magonjwa hayo na kutoa matibabu bure kwa Wananchi ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza, kwani jamii yenye Afya bora inaweza kufanya kazi kwa bidii na kuufukuza umaskini.

“Nitoe rai kwa Wananchi wa Bagamoyo kuzingatia kula lishe bora kwa wakati, kufanya mazoezi, kufanya vipimo kuangalia hali za Afya zetu mara kwa mara na kuepuka matumizi ya sigara na vilevi vingine kama Pombe kupitiliza kwani mtindo huu wa maisha unaweza kusaidia kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari, Siko seli, shinikizo la damu, uoni hafifu, udumavu, utapiamlo, magonjwa ya meno n.k” Amesema Bi. Kasilda

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Fatuma O. Latu akizungumza katika kumbukizi hiyo amewasisitiza Wananchi kuacha hofu ya kupima Afya zao kwa hiyari mara kwa mara bila kusubiri kufanya hivyo pale wanapokutwa na maradhi na kuwashauri pia kujenga utaratibu wa kujitolea damu kwa hiyari ili benki ya damu katika Vituo vya kutolea huduma za Afya isikaukiwe damu.

“Wengi wetu tumekuwa waoga sana wa kufanya vipimo kutazama hali zetu za Afya, jambo hili hupelekea wengi kufika Hospitali kupatiwa matibabu wakiwa katika hali mbaya za ugonjwa ambapo wangekuwa na utaratibu wa kujitazama Afya mara kwa mara wangeepuka kufikia hatua mbaya ya ugonjwa na kupunguza gharama kubwa za matibabu” Amesema Mkurugenzi Fatuma

Anaongeza Mkurugenzi Fatuma, “Niwaombe Wananchi wa Bagamoyo pia kujenga utaratibu wa kujitolea damu ili kuimarisha benki ya damu katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na katika Vituo vingine vya kutolea huduma za Afya kwani benki ya damu inapokuwa ya uhakika Wananchi pia wanakuwa na uhakika wa huduma hiyo ambayo mara nyingi huwa ni ya dharura yasiyoweza kusubiri pale mgonjwa anapoihitaji”.

Bi. Rehema Kingu ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na mratibu wa maadhimisho hayo amesema tafiti zinaonesha kuwa mnamo Mwaka 2019 magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi, na inakadiriwa kuwa Asilimia 60 ya vifo vyote Duniani vilivyotokea, vilisababishwa na magonjwa yasiyoambukiza na Asilimia 43 ya watu Duniani wanaugua magonjwa yasiyoambukiza.

“Kama juhudi hazitachukuliwa ni Dhahiri kuwa idadi ya vifo vitokananvyo na magonjwa yasiyoambukiza Duniani itaongezeka hadi kufikia Asilimia 73 ya vifo vyote ifikapo Mwaka 2020, hata hivyo takwimu pia zinaonesha kuwa katika Nchi yetu ya Tanzania hadi kufikia Mwaka 2019 Asilimia 31 ya vifo vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza” Amesema Bi. Rehema

Kwa Mwaka 2020 kauli mbiu ya magonjwa yasiyoambukiza inasema “Tutembee pamoja katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza”



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo