• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAHAMIAJI HARAMU 49 WAKAMATWA BAGAMOYO, WAPIMWA CORONA KABLA YA KWENDA MAHABUSU

Posted on: March 19th, 2020


Wahamiaji haramu 49 wamekamatwa  Wilayani Bagamoyo usiku wa kuamkia tarehe 19/03/2020 Wahamiaji hao haramu wamekamatwa na raia wema wakishirikiana na Jeshi la Polisi Wilayani Bagamoyo katika Kijiji cha Kidomole Kata ya Fukayosi.


Raia hao 49 wa Ethiopia wamekiri kuingia nchini kinyume cha sheria kwa kupitia pwani ya Bagamoyo wakitumia majahazi ikiwa lengo lao ni kuelekea Afrika kusini.


Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa amesema kuwa walipokea taarifa toka kwa raia wema juu wa uwepo wa kundi la watu wasiofahamika katika Kijiji cha Kidomole kilichopo Kata ya Fukayosi, na baada ya taarifa hiyo hatua za haraka zilichukuliwa na Jeshi la Polisi Wilayani humo kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji hao haramu 49.


Mhe. Zainab ameongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ulioingia Nchini, tumeona ni vyema kuwafanyia vipimo vya awali vya kiafya wahamiaji hawa ili kujiridhisha kuwa wako salama kabla hawajaendelea na taratibu zingine za kimahakama.


"Hivyo tumewaleta hapa katika Kituo cha Afya Matimbwa ili kuwaangalia Afya zao kwanza hasa joto la mwili kuwaangalia kama wana homa kali, kama wana dalili zozote za kikohozi, au mafua makali, kisha wataendelea na taratibu zingine za kisheria, Alisema Kawawa.


 “Niwapongeze Wananchi wema waliosaidia kukamatwa kwa wahamiaji hawa haramu, lakini pia nitoe rai kwa Wananchi wote wa Bagamoyo kuwa wazalendo na kuacha kabisa vitendo vya kuwasaidia wahamiaji haramu na kufanya Bagamoyo kuwa uchochoro wa kupita kuelekea Nchi jirani, kuwasaidia wahamiaji haramu kupita Bagamoyo na kokote Nchini kunahatarisha usalama wa Nchi yetu hasa kipindi hiki ambacho Nchi nzima inapambana na mlipuko wa ugonjwa huu wa Corona” Alisema Mhe. Zainab Kawawa.


Jeshi la Polisi Wilayani Bagamoyo limekuwa likiwakamata wahamiaji haramu hasa wanaotoka Nchini Ethiopia na kuingia Nchini kwa kutumia pwani ya Bahari ya Hindi, wakiwa njiani kuelekea Nchi jirani na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria ikiwa ni katika kupambana na uingiaji wa makundi haya ya wahamiaji haramu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo