• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAHUDUMIENI WANANCHI KWA MOYO MWEUPE

Posted on: March 25th, 2020


Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Kasilda Mgeni, mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ili kujionea namna huduma zinavyotolewa na wagonjwa wanavyohudumiwa hospitalini hapo.


Bi. Kasilda, ameyasema hayo alipofanya ziara hiyo maalum iliyokuwa na lengo la kuhamasisha utoaji huduma bora kwa wananchi ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya huduma zinazotolewa hospitalini hapo, pia kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili watumishi na watoa huduma.



“Niwapongeze watoa huduma wetu, madaktari na wauguzi kwa huduma nzuri mnazowapatia wananchi wanapofika hapa Hospitali wakihitaji huduma za Kiafya, hakika mnajitahidi, lakini niwakumbushe kuhakikisha mnatoa huduma hizi kwa moyo mweupe, kwa kujitoa na kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa umma, kila mtu awajibike kwenye eneo lake kwa weledi mkubwa hii itasaidia sana kupunguza malalamiko kwa wananchi tunaowahudumia” Amesema Bi. Kasilda



Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Dkt. Aliko Mbughi amesema, kama Watumishi, wanajitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa Wananchi na kwa wakati licha ya changamoto mbalimbali walizonazo kama uhaba wa vifaa tiba na uchakavu wa majengo ambazo wamekuwa wakizitatua kwa kadiri fedha zinavyopatikana na kuendelea kutenga kwenye bajeti yao ya Idara ya Afya kila Mwaka.


Katika Ziara hiyo pia Katibu tawala, Bi. Kasilda mgeni pia alipata fursa ya kuona baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi za wanawake, wanaume na watoto, kuwapa pole na kuwatia moyo huku wagonjwa hao wakionesha kufurahia jinsi huduma za Afya zilivyoboreshwa hospitalini hapo.


Wakati huo huo, Bi. Kasilda ametumia fursa hiyo kusikiliza baadhi ya kero za Watumishi wa Hospitali hiyo ambapo wengi wamelalamikia upandishwaji wa madaraja kusua sua hivyo akaahidi kulichukua suala hilo na kwenda kulifanyia kazi, ili watumishi hao nao wafurahie kutumika kama Watumishi wa umma na kuimarisha utoaji huduma bora kwa jamii wanayoihudumia.


Katika ziara hiyo Bi. Kasilda ametembelea eneo la mapokezi (OPD), Jengo la kupokelea wagonjwa wa dharura, duka la dawa la jamii, dirisha la bima, kitengo cha X-ray, Jengo la upasuaji, Wodi za wanawake, wanaume na watoto, Jengo la methadone, jengo la kuhifadhia maiti, maabara, kitengo cha macho na kitengo cha utoaji nasaha na kupima (CTC) ambako kote ameongea na Watumishi wa vitengo hivyo akiwasisitiza juu ya utoaji huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia sharia, taratibu na kanuni za Utumishi wa umma.



maendeleo, kuzungumza na wananchi na kusikiliza changamoto na kero zao ili kuyapatia majawabu.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo