• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAKULIMA BIDP WALIA NA MKANDARASI

Posted on: February 9th, 2019

Wakulima wa mpunga wapatao 28 wanachama wa skimu ya Umwagiliaji BIDP maarufu kama Skimu ya Jitegemee iliyopo Sanzale, Kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo, wamemlalamikia Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara na mifereji ya maji katika skimu hiyo kwa kuwatia hasara kwa kusua sua kwa utekelezaji wa mradi huo.

Mkandarasi huyo toka kampuni ya musons engineers alianza kutekeleza mradi huo Mwezi April 2018 na alitarajiwa kukamilisha mradi mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2018 lakini hadi sasa hajakamilisha mradi huo na anaendelea kuutekeleza akiwa katika kipindi cha adhabu ambacho pia kinakwisha ifikapo tarehe 18 Februari, 2019.

Wakulima hao 28, waliwasilisha malalamiko yao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waheshimiwa madiwani ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Hapsa Kilingo ambaye aliongoza wajumbe wa kamati hiyo waliofuatana na Wataalam wa Halmashauri kuutembelea na kuukagua mradi huo wa ujenzi wa mifereji na barabara katika Skimu ya Umwagiliaji ya Tegemeo mapema jana.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake wa skimu ya Tegemeo, mmoja wa wakulima (jina limehifadhiwa) anayefanya shughuli zake za kilimo katika Skimu hiyo kwenye kitalu gh amesema, yeye na wakulima wenzake wa kitalu gh ndio wahanga wakubwa zaidi, kwani tangu msimu wa pili wa kilimo uanze hawajafanikiwa kabisa kupata maji katika mashamba yao, kutokana na mkandarasi kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati, hususani ujenzi wa mifereji ya kupeleka maji katika kitalu hicho, hali iliyopelekea wakulima 28 wa kitalu gh kupata hasara kubwa ya kuunguliwa na mazao yao.

“Wakati wenzetu wakikaribia kuvuna mpunga katika mashamba yao, sisi hatuna kabisa matarajio hayo ya kupata chakula katika msimu huu, ni maumivu makubwa sana kwa mkulima kulima kisha akakosa mavuno kwa sababu za uzembe tu wa mkandarasi aliyeamua kufanya kazi bila kuzingatia mahitaji halisi ya wakulima lakini pia kwa kusua sua sana hivyo kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati, niwaombe viongozi watusaidie kuhakikisha mradi huu unakamilika ili tuondokane na changamoto hizi” Anaongeza Mkulima huyo.

Nae diwani wa Kata ya Magomeni unakotekelezwa mradi huo Mhe. Mwanaharusi Jarufu akizungumza katika Ziara hiyo ameonesha kutoridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mifereji na barabara katika Skimu hiyo, na kueleza kwamba mradi umetekelezwa chini ya kiwango na ni vyema Mamlaka zinazohusika kufika katika mradi huo na kuukagua kuona kama mradi umetekelezwa katika kiwango kinachotakiwa, kwani hayuko tayari kuona fedha za Serikali zinapelekwa katika Kata anayoiongoza na kisha fedha hizo zisifanye kile kilichotarajiwa na Serikali.

Akizungumza na Wakulima hao mara baada ya kukagua mradi huo na kusikiliza kero za wakulima wa skimu hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Mhe. Kilingo amewaasa wakulima hao kuwa watulivu na wavumilivu wakati kamati yake na Ofisi ya Mkurugenzi ikiendelea kushughulikia suala lao kwa haraka kwa kufanya mazungumzo na mkandarasi ili akamilishe mradi huo mapema iwezekanavyo.

Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira jana imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Sekta za Kilimo na Ufugaji ikiwa ni katika utaratibu wake wa kawaida wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kila robo.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo