• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WALIMU NA WANAFUNZI WALIONG'ARA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA CHA PILI WAZAWADIWA

Posted on: May 2nd, 2018



Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imefanya kikao cha tathmini ya kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne na mtihani wa kujipima wa kidato cha pili iliyofanyika mwishoni mwa mwaka 2017, na kuwazawadia walimu, shule na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani hiyo.
Kikao hicho kilichofanyika Aprili 30, 2018 katika Shule ya Sekondari Bagamoyo, kilihudhuriwa na Walimu, Wakurugenzi wa Shule za Sekondari, Wawakilishi wa taasisi za kifedha na wadau mbalimbali wa elimu ndani ya Halmashauri, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Erica Yegela.
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ina jumla ya Shule 21 za Sekondari, kati ya hizo 12 ni binafsi na 9 za Serikali, na kwa mwaka 2017, Shule 18 zilishiriki kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari (kidato cha nne), ambapo jumla ya Wanafunzi 1,667 walifanya mtihani huo, kati ya Wanafunzi 1,680 walioandikishwa, kati yao Wasichana ni 949 na Wavulana 718 sawa na asilimia 99.23% ya Wanafunzi walioandikishwa.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Idara ya elimu msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Violeth Mlowosa amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kati ya Halmashauri 195 nchini, katika mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2017, baada ya kupata GPA ya 3.29 ambapo kwa mwaka 2016 ilishika nafasi ya 17.
Anaongeza, Wanafunzi waliofaulu walikuwa 1,250 (Wavulana 525 na Wasichana 727) sawa na 74.49%, lakini Wanafunzi 291 (Wavulana 114 na Wasichana 177) sawa na 17.46% walishindwa mtihani huo na Wanafunzi 126 (Wavulana 81 na Wasichana 45) sawa na 7.55% matokeo yao yalizuiliwa.
Anasema, kwa upande wa mtihani wa upimaji wa kidato cha pili (FTNA) jumla ya wanafunzi 2022 walifanya mtihani kati yao Wavulana 826 na Wasichana 1162. Jumla ya Wanafunzi 214 (Wavulana 98 na Wasichana 116) walishindwa na hivyo kutakiwa kurudia kidato cha pili Mwaka 2018.
Mgeni rasmi katika kikao hicho Bi. Erica Yegela ambae pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, akizungumza na washiriki wa kikao hicho amesema, ni vyema kuweka mkakati maalum wa kuboresha ufaulu kwa kuongeza mbinu bora za ufundishaji, pia kuanzishwa kwa mikutano ya walimu, wazazi na wanafunzi watakaokaa na kujadili kwa pamoja changamoto anazokumbana nazo Mwanafunzi zinazopelekea kudunisha ufaulu wa mwanafunzi, kisha kumsaidia kutatua changamoto hizo ili aweze kufanya vizuri shuleni.
Akawataka pia walimu kuzingatia ufundishaji kwa vitendo (practical) zaidi na kuacha kutegemea kufundisha nadharia peke yake hasa kwa masomo ya Sayansi.
Vilevile akawaasa walimu juu ya kuzingatia nidhamu na weledi na akaishauri Ofisi ya Mkurugenzi kuwapa nafasi walimu wanaotaka kujiendeleza kimasomo kwa kuwaweka katika mpango wa bajeti bila kuwa na urasimu wowote.
Wakati huo huo, Bi. Yegela akawapongeza pia sekta binafsi na mashirika ya dini yaliyowekeza katika sekta ya elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akiwanzadi kuwa Shule zao ndizo zinazofanya vizuri zaidi na kupelekea Halmashauri yetu kupata nafasi ya kuongoza Kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2017.
Akaongeza, nidhamu na maadili mema ni chachu ya mafanikio na ufaulu wa wanafunzi, hivyo vijana wanaojiunga na chama cha skauti mashuleni wasipuuzwe,m watiwe moyo, waelekezwe na kuongozwa vyema kwani mafunzo wanayaoyapata kupitia chama hiko cha skauti yanawasaidia pia kujenga nidhamu na afya.
Akatumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashuri, Mkuu wa idara ya Elimu sekondari, Wanafunzi, Walimu, Wazazi, Walezi na wadau mbalimbali wa elimu katika halmashauri
Zawadi za vyeti na fedha taslimu zilitolewa kwa Walimu, Wanafunzi na Shule zilizofanya vizuri zaidi katika masomo ya Sayansi na Sanaa kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne iliyofanyika novemba 2017, na mitihani ya kujipima ya kidato cha pili ambayo pia ilifanyika mwishoni mwa Mwaka jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo