• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WALIMU WANAODANGANYA UMRI WA KUSTAAFU KUKIONA

Posted on: May 30th, 2018


Na Adili Mhina,

Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bibi Winifrida Rutahindurwa amewaonya waalimu wanaofanya udanganyifu kwa lengo la kujiongezea muda wa kuwepo katika utumishi wa Umma licha ya muda wao wa kustaafu kuwa umefika.

Bibi Rutahindurwa alitoa kauli hiyo leo Mei 30 , 2018 mjini Bagamoyo alipokutana na waalimu wakuu na wakuu wa shule wa wilaya za Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kutoa elimu juu ya wajibu wa walimu wakuu na  wakuu wa shule kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu na. 25 ya mwaka 2015.

Alieleza kuwa wapo baadhi ya walimu waliobadilisha taarifa zao na zikaingizwa kwenye stakabadhi za mishahara kwa lengo la kujipunguzia umri ili kuendelea kuwepo kazini kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

“Kuna baadhi ya waalimu wanajifanya hawakumbuki walizaliwa mwaka gani wakati walijaza mikataba wakati wanaaza ajira na wengi wao wamebadilisha taarifa zao na kujipunguzia umri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria”.

 “Nimegundua kuwa wapo baadhi ya waalimu ambao pindi walipoagizwa na waajiri wao kupeleka taarifa zao binafsi walijifanya hawakumbuki mwaka waliozaliwa, wakaamua  wakajipunguzia umri ili wendelee kuwepo kazini kwa muda mrefu zaidi”, alisema Bi. Rutahindurwa.

Alitoa ufafanuzi kuwa mwalimu atakapoandikiwa kibali cha kustaafu, pamoja na kuangalia stakabadhi ya mishahara kigezo kikubwa kitakachotumika kuangalia umri halisi wa mwalimu kustaafu ni taarifa alizojaza awali wakati anaanza ajira yake.

Bi. Rutahindurwa aliweka bayana kuwa yapo madhara kwa mwalimu ambaye muda wake wa kustaafu utafika lakini akaendelea kuwepo kazini kwa kuwa watakapodai mafao yaake atakatwa mishahara yote aliyolipwa kwa kipindi chote alichofanya kazi baada ya muda wake wa halali kupita.

Alisisitiza,“ naomba muwaeleze walimu wote katika shule zenu kuwa utakapoandikiwa kibali cha kustaafu sisi tunaangalia zaidi taarifa zako ulizojaza wakati unaajiriwa. Ikibainika umedanganya utachukuliwa hatua kwa kuwa umemwibia mwajiri”.

Alieleza kuwa kwa walimu wote ambao hawakumbuki taarifa walizojaza kwenye mikataba yao wakati wa kuanza kazi wawasiliane na ofisi za tume ya utumishi wa walimu katika Wilaya zao ili kupata uhakika wa tarehe zao za kustaafu.

Akaongeza, kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa walimu namba 25 ya mwaka 2015, wao ndio mamlaka ya kwanza ya nidhamu kwa walimu. Hivyo, wanapaswa kuwashauri na kuwaelimisha walimu badala ya kukaa na kusubiri wafanye makosa ili wawachukulie hatua.

Kwa upande wao walimu walionesha kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuondoa usumbufu kwa mwalimu pale anafuatilia masuala yake ya mafao mara baada ya kustaafu.

Walimu hao wametoa pongezi kwa katibu wa TSC kwa jitihada kubwa anazofanya katika kuhakikisha mashauri ya waalimu yanafanyiwa kazi kwa wakati na maamuzi yanatolewa kwa muda muafaka.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo