• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WANAFUNZI 148 WA SHULE YA SEKONDARI KINGANI WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI SOKO LA SAMAKI

Posted on: April 26th, 2018


Wanafunzi wapatao 148 toka Shule ya Sekondari Kingani iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, wameshiriki kuadhimisha sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuendesha zoezi la Usafi katika Soko la Samaki lililopo Pwani ya Bagamoyo mjini.

Wanafunzi hao wa Kidato cha kwanza hadi cha nne ni wanachama ya Klabu ya wapinga Rushwa Shuleni hapo ambayo mbali na kufanya uhamasishaji na uelimishaji kwa Wanafunzi wenzao juu ya madhara ya Rushwa pia hujihusisha na masuala ya utunzaji wa mazingira.

Caroline Kabile Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kingani ni Mwenyekiti wa Klabu hii na hapa anabainisha “Leo tumeadhisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini Klabu yetu kwa kuona umuhimu wa tukio hili, tumeamua kuja kufanya usafi katika soko hili la Samaki, lakini pia tumetumia fursa hii kuwaelimisha wavuvi na wafanya biashara wa eneo hili kuzingatia Usafi wanapokua katika shughuli zao za kila siku katika maeneo haya ili kuepuka madhara tanayoweza kutokea kwa wao kufanya shughuli zao katika eneo chafu, hasa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na mengineyo yanayosababishwa na uchafu”.


Nae Afisa usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Cleophace Murugwa akizungumza na wanafunzi hao kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, amewashukuru Wanafunzi hao kwa moyo wao wa kujitolea lakini pia kutambua umuhimu wa kutunza mazingira na uelimishaji umma kwa njia ya vitendo namna ya kutunza mazingira yao na kuzingatia usafi na kuwaasa kutoishia hapo bali kuendeleza hulka hiyo hata wanapokuwa Shuleni na majumbani mwao.


Wakati huo huo Taasisi ya Elimu ya ADEM iliyopo Bagamoyo nao wameadhimisha  miaka 54 ya Muungano kwa kufanya zoezi la upandaji miti 200 katika eneo la Taasisi yao.


Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dr. Siston Mgula akizungumza wakati wa zoezi hilo chuoni hapo amesema “Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Joseph Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na watanzania wote kwa kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini pia akatumia fursa hiyo kuwaasa Walimu wanaosoma katika Taasisi hiyo kuwa mabalozi wazuri wa utunzaji mazingira pindi watakapomaliza masomo yao chuoni hapo na kurudi katika vituo vyao ya kazi.


Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitiwa saini rasmi na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar na Maadhimisho ya Muungano kitaifa yamefanyika Mkoani Dodoma katika Uwanja wa Jamuhuri mapema leo Asubuhi na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo