• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WANAFUNZI BAOBAB WAFADHILI MAGODORO 30 KITUO CHA AFYA KEREGE

Posted on: November 7th, 2018


Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita, toka shule ya Sekondari Baobab iliyopo Mapinga Wilayani Bagamoyo, wametoa msaada wa magodoro 30 kwa ajili ya wodi ya wzazi katika kituo kipya cha Afya Kerege.

Vijana hao takribani 50 ni Wanafunzi wanaounda klabu ya UN-CLUB, (Klabu ya Vijana ya Umoja wa Mataifa) iliyoundwa shuleni hapo ikiwa na lengo la kuwafundisha Wanafunzi kujitoa na kusaidia jamii katika nyanja mbali mbali lakini pia huwasaidia wanafunzi wenzao wenye mahitaji maalum Shuleni hapo.

Akizungumza katika risala maalum ya Wanafunzi hao, Debora ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule hiyo ya Baobab amesema, wamekuwa na utaratibu maalum wa kuhamasishana kupitia klabu yao na kutoa misaada ya kijamii kwa jamii ya Kitanzania yenye mahitaji kama vile vituo vya kulelea watoto yatima, n.k

“Tumekuwa tukitoa misaada ya kijamii katika vituo vya kulelea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu. Hadi sasa tumefanikiwa kuifikia mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. Baadhi ya vituo tulivyovipatia msaada ni kituo cha Mother Theresa na kituo cha CHAKUWAMA vyote vya Jijini Dar Es Salaam, Kituo cha Green pastures kilichopo Bagamoyo, Pwani na Kituo cha Mihayo kilichopo Morogoro kinachotoa huduma na kulea watoto wenye ulemavu wa ngozi. Tumekuwa tukitoa misaada ya vyakula kama vile mahindi, sukari, mafuta ya kupikia, mchele, unga na sabuni. Na mara hii tumeguswa kuja kukisaidia kituo hiki cha Afya Kerege, ikiwa ni katika kusaidia jamii yetu inayotuzunguka kwa kidogo tunavyojaliwa na Mwenyezi Mungu”, Anasema Debora.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Baobab Mwl. Venance Hongoa amesema Wanafunzi hao wa Klabu ya UN- CLUB wameamua kutoa msaada huo wa magodoro 30 katika kituo hiko cha Afya Kerege ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli za kuboresha na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za Afya nchini na kuhakikisha inapunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwa kujenga vituo vipya vya Afya katika kila Halmashauri Nchini.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu amewashukuru sana Wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari Baobab kwa kuwa na moyo huo wa kujitolea kwa jamii, lakini pia akaupongeza uongozi wa Shule hiyo kwa kuwafundisha vijana hao kuwa wazalendo na kuisaidia jamii yao inayowazunguka.

“Kituo hiki cha Afya Kerege ni moja ya kati ya Vituo vipya 44 vya Afya Nchini, vilivyojengwa katika awamu ya kwanza ya uimarishaji na uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya unaofanywa na Serikali ya Awamu ya tano, ambapo kilishika namba 1 kwa ubora kati ya Vituo vyote 44 vilivyojengwa katika awamu hiyo ya kwanza. Kituo cha Afya Kerege kimeshaanza kutoa huduma kwa Wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo japo hazitoshi lakini kwa msaada huu mliotupatia leo mmetusaidia kupiga hatua kubwa sana ya utoaji huduma katika Kituo hiki cha Afya Kerege” Amesema Bi. Fatuma Latu.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Kerege ulianza mnamo Mwezi Oktoba 2017 na kukamilika Mwezi Machi 2018 kwa ufadhili toka Serikali Kuu na umegharimu jumla ya Shilingi Mil. 500.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo