• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WANANCHI TUJITOKEZE KUSAIDIA KUPATIKANA KAYA MASIKINI..

Posted on: April 19th, 2021

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo  Mhe. Mohamedi Usinga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kusaidia zoezi la kuzipata kaya masikini kuweza kuingia kwenye mpango wa kunusuru kaya masskini (Tasaf).

Hayo ameyasema wakati wa kikao kazi  cha kujenga uelewa kuhusu mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili kwa viongozi,watendaji na wawezeshaji tarehe 19 Aprili 2021kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashuri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Mhe Usinga amewataka wananchi kujitokeza kwenye mikutano yote ili walengwa waweze kupatikana kwa haki bila kuwepo upendeleo na uonevu wakati wa utafutaji wa kaya maskini katika sehemu zote ambazo zitapitiwa na mpango huu.  ‘’Natoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika mikutano yote ambayo itaitishwa na viongozi kwa ajili ya kufanya zoezi la upatikanaji wa kaya maskini wajitokeze kwa wingi ili kusaidia zoezi hili liende kama lilivyo pangwa’’alisema  Mwenyekiti wa Halmashauri.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ametoa wito kwa Tasaf kusimamia na kufanya ufuatiliaji ili kuweza kuona namna ambavyo wananchi wanapata stahiki ambazo wamepanga kuzipata na kuboresha maisha yao ili yaweze kubadirika kupitia mfuko huo wa Tasaf.

Nae mratibu wa kunusuru kaya masikini Tasaf katika Halmashauri ya Bagamoyo Bw. Deionises Gozbert Mahilane amesema kuwa, mafunzo yanakwenda vizuri  ambapo nia na lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo ili kuweza kujua ni taratibu gani zitatumika kuwapata walengwa wa kaya maskini  katika vijiji  na vitongoji vyote.

Mratibu huyo wa Tasaf Wilaya amesema, mpango uliopita uliwapata walengwa kwa asilimia 70 katika vijiji vyote  na kwa sasa  watachukuliwa wale  asilimia 30 waliobaki awamu ya kwanza kwa vijiji saba vya  Halmashauri  Wilayanya Bagamoyo vilibaki  ili kukamilisha asilimia 30 zilizobaki.  ‘’Katika Halmashauri ya Bagamoyo kuna vijiji saba vilivyobaki ambavyo ni kata ya Fukoyosi kijiji cha kidomole,kata ya yombo kijiji cha yombo kata ya Kiromo kijiji cha Kiromo, na Kitopeni,kata ya Zinga kijiji cha Mlingotini, kwa Mazinga na Pande’’alisema Mratibu wa Tasaf.

Tasaf imeandaa utaratibu wa kufikia Vijiji/Mitaa/Shehia ambazo hazikufikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya mpango utambuzi wa kaya masikini utafanywa na wanajamii kupitia mikutano  ya vijiji/mitaa/shehia kwa usimamizi wa wawezeshaji kutoka mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRATIBU WA MRADI WA MARCOSIO TAFIRI AONGOZA WASHIRIKI WA WARSHA KUTEMBELEA WAVUVI WILAYA YA BAGAMOYO...

    May 29, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI...

    May 23, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI AKAGUA MWENENDO WA UANDIKISHAJI...

    May 18, 2025
  • MKUU WA WILAYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UTALII..

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo